TANGAZO


Thursday, November 29, 2012

Viongozi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wazindua barabara ya Arusha - Namanga - Athi River

 

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi Kenya Jumatano, Novemba 28, 2012 tayari kuhudhuria sherehe za ufunguzi wa barabara ya Arusha-Namanga-Athi River pamoja na Mkutano wa Wakuu wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki utaozungumzia maendeleo ya miundombinu. Kiongozi wa Jumuiya ya Waislamu wa Ismailia Mtukufu Aga Khan naye alikuwepo hapo uwanjani hapo. (Picha zote na Ikulu)
 
Rais Jakaya Kikwete, akisalimiana na viongozi wengine wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki wakati wa hafla hiyo.
Rais Jakaya Kikwete, akiwa na Marais wenzake wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, wakati wa hafla ya uzinduzi huo.
Rais Jakaya Kikwete akisaini kitabu cha wageni wakati wa hafla hiyo.
Baadhi ya Mawaziri na Makatibu wakuu wa Tanzania waliohudhuria sherehe za uzinduzi rasmi wa barabara ya Arusha – Namanga – Athi River yenye urefu wa kilometa 104.4 kwa upande wa Tanzania.
Rais Jakaya Kikwete akitoaa hotuba yake wakati wa uzinduzi wa barabara hiyo
 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipanda mti wakati wa uzinduzi wa barabara hiyo.
 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na viongozi wenzie wa nchi wanachama za Jumuiya ya Afrika Mashariki wakikata utepe kwa pamoja kuzindua rasmi wa Barabara ya Arusha – Namanga – Athi River yenye urefu wa kilometa 104.4 kwa upande wa Tanzania.
 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na viongozi wenzake wa nchi wanachama za Jumuiya ya Afrika Mashariki wakifurahia mara baada ya kuzindua rasmi ujenzi wa barabara hiyo kwa kukata utepe.
 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na viongozi wenzie wa nchi wanachama za Jumuiya ya Afrika Mashariki wakiwa katika picha ya pamoja na wadau mbalimbali waliofanikisha ujenzi wa barabara ya Arusha – Namanga – Athi River.

No comments:

Post a Comment