TANGAZO


Thursday, November 29, 2012

Kesi ya walioathirika na milipuko ya mabomu 2009 Mbagala yahamishiwa Baraza la Usuluhishi

KESI ya madai ya fidia iliyofunguliwa na wakazi wa Mbagala, Wilayani Temeke, jijini Dar es Salaam walioathirika na mabomu mwaka 2009 imehamishiwa Baraza la Usuluhishi ili kutafuta muafaka kati yao na Serikali.
 
Baraza la usululishi ili kufanya mazungumzo baina ya pande hizo mbili yaani Serikali na wananchi hao.
Akitoa maamuzi hayo jijini hivi karibuni, baada ya wikili wa serikali, Mikidadi Rashid, kuwasilisha ombi la serikali ya kutaka shauri hilo lipelekwe katika Baraza hilo, Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu, Dk. Fauzi Twaib, alisema Mahakama inakubaliana na ombi hilo.
Shauri hilo limepangwa kuanza kusikilizwa na kikao cha Baraza hilo la Usuluhishi kuanzia Februari 27, 2013.
Jaji Twaibu alisema pande zote zimekubali kupeleka kesi hiyo kwenye baraza hilo, hivyo Mahakama inabariki hatua hiyo kwaza na baada ya majadiliano hayo kushindika ndipo itaazwa kusikilizwa upya.
Akizungumzia hatua hiyo Katibu msaidiza wa waathirika hao Alvan Agustino .alisema wameafiki hatua hiyo ya Mahakama ya kutaka kukaa meza ya usululishi na Serikali na kama itashindikanika kupata muafaka basi kesi itasikilizwa upya.
Alisema Kesi hiyo namba 181 ya 2011 iliifunguliwa na wakazi hao kutokana na kutoridhishwa na kiwango cha fidia ambacho walilipwa na serikali baada ya mali zao zikiwemo nyumba kuathiriwa na mabomu yaliyolika katika kambi ya Mbagala Aprili 2009.
Alisema watu zaidi ya 76 hawakuridhishwa na fidia hiyo ambapo serikali hawakukubali kulipa zaidi na wakaamua kufungua kesi Mahakama kuu na kuidai serikali sh. bilioni moja.

No comments:

Post a Comment