TANGAZO


Tuesday, November 20, 2012

Tuzo za Walimu Bora Tanzania 2013

Mwenyekiti wa Bodi ya Tuzo kwa Walimu bora Tanzania, Profesa Emanuel Mjema, akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, kuhusu utoaji tuzo kwa walimu watakaofanya vizuri katika ufundishaji masomo mbalimbali nchini. Kulia ni mjumbe wa bodi ya tuzo hiyo, Zuwena Kipingu. (Picha zote na Kassim Mbarouk)

Baadhi ya waandishi wa habari, wakiandika maelezo yaliyokuwa yakitolewa na Mwenyekiti wa Bodi ya Tuzo kwa Walimu bora Tanzania, Profesa Emanuel Mjema (hayupo pichani), wakati alipokuwa akizungumza nao, Dar es Salaam leo, kuhusu utoaji wa tuzo kwa walimu watakaofanya vizuri katika ufundishaji masomo mbalimbali nchini.

Mwenyekiti wa Kamati ya Usaili na Vigenzo katika kuwapata walimu bora, Dk. Wilson Charles, akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari katika mkutano huo jijini leo. Katikati ni Mwenyekiti wa Bodi ya Tuzo kwa Walimu bora Tanzania, Profesa Emanuel Mjema na kulia ni mjumbe wa bodi ya tuzo hiyo, Zuena Kipingu.
 
Mwenyekiti wa taasisi ya Education and Expendition Agency Association (EEAA), Clemence Kambengwa, ambao ni waandaaji wa tuzo hizo, akifafanua jambo kwa waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, wakati wa mkutano huo. Kushoto ni mjumbe wa bodi ya tuzo hiyo, Zuwena Kipingu na katikati ni Mkurugenzi wa Masoko wa benki ya Posta, Adrew Chimazi.

Mkurugenzi wa Masoko wa benki ya Posta, Adrew Chimazi, akizungumza katika mkutano huo, Dar es Salaam leo. Kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Tuzo kwa Walimu bora Tanzania, Profesa Emanuel Mjema na katikati ni mjumbe wa bodi ya tuzo hiyo, Zuena Kipingu.

No comments:

Post a Comment