Mchezaji Emmanuel Okwi wa Simba akimtoka Ally Ahmed wa Toto African ya Mwanza wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom, uliochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo. Toto imeshinda bao 1-0. (Picha zote na Kassim Mbarouk)
Mchezaji Emmanuel Okwi wa Simba akimtoka Robert Magadula wa Toto African ya Mwanza wakati wa mchezo huo wa Ligi Kuu ya Vodacom, uliochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo.
Paul Ngalema wa Simba akimtoka Mussa Said 'Kimbu' wa Toto African ya Mwanza, wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom, uliochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo.
Mashabiki wa Simba wakifuatilia mchezo kati ya timu hiyo na Toto African ya Mwanza.
Mrisho Ngassa wa Simba akitafuta mbinu ya kumtoka Ally Ahmed wa Toto African ya Mwanza, wakati wa mchezo huo, Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam leo.
Erick Kyaruz wa Toto African ya Mwanza, akipiga mpira kichwa huku akizongwa na Haruna Chanongo wa Simba katika mchezo huo.
Wachezaji Amri Kiemba (mbele), Felix Sunzu (kushoto), wote wa Simba, wakiwania mpira wa juu na Evarist Maganga wa Toto African katika mchezo huo wa Ligi Kuu ya Vodacom, uliochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo jioni. Toto ilishinda bao 1-0.
Peter Mutabuzi wa Toto African ya Mwanza, akimiliki mpira huku akifuatwa na Felix Sunzu wa Simba wakati wa mchezo huo.
Amri Kiemba wa Simba, akikatwa kwanja na James Magafu wa Toto African.
Mpaka mwisho wa mchezo, ubao wa matangazo ulikuwa unaonesha Toto African ya Mwanza bao 1 na Simba 0.
Wachezaji wa Toto African wakiwa wamembeba kocha wao msaidizi, Athuman Bilal baada ya kushinda mchezo huo kwa bao 1-0 hadi mwisho wa mchezo.
No comments:
Post a Comment