Baadhi ya Wananchi wa Kjiji cha Kidagoni, Wadi ya Kidoti wakisikiliza hotuba ya Kamishna wa Elimu Zanzibar (hayupo pichani) katika sherehe za kukabidhiwa vifaa mbalimbali vya Shule ya Kidagoni. jana.
Wanafunzi wa Shule ya Kidagoni, Mkoa wa Kaskazini, Wadi ya Kidoti wakiwa katika banda lao la Shule ambalo wakisomea kabla ya Serikali kuwajengea jengo jipya la Shule hio (lililo upande wa kulia) . Kijiji hicho kinakabiliwa na matatizo mbalimbali, ikiwa pamoja na barabara yakufikia huko. Maji safi na salamana kituo cha Afya.
Naibu Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Ofisi ya Zanzibar Mcha Hassan Mcha (kulia), akitoa hotuba ndogo baada ya kukabidhi Msaada wa Vifaa mbalimbali vya Shule ya Kidagoni na kuahidi kuwafikishia maji safi Shuleni hapo. Kulia kwake ni Kamishna wa Elimu Zanzibar, Maryam Abdalla Yussuf.
Kamishna wa Elimu Zanzibar Maryam Abdalla Yussuf.akifafanua jambo wakati akitoa hotuba baada ya Kupokea Msaada wa Vifaa mbalimbali vya Shule ya Kidagoni ilioko Mkoa wa Kaskazini, Wadi ya Kidoti. Kushoto yake ni Naibu Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) Ofisi ya Zanzibar Mcha Hassan Mcha na kulia kwake ni Afisa Utumishi Mwandamizi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA), Ofisi ya Zanzibar, Haura Kassim. (Picha zote na Yussuf Simai - Maelezo Zanzibar)

No comments:
Post a Comment