Na Francis Godwin,Iringa
BAADA ya mfanyabiashara na kada wa chama cha mapinduzi (CCM) mkoa wa Iringa Salim Abri Asas kukabidhi mifuko 200 ya saruji yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 3 ,mfanyabiashara maarufu nchini Subash Patel ameungana na Asas kwa kuunga mkono jitihada za mkuu wa wilaya ya kilolo katika mkoa wa Iringa Gerald Guninita kwa kwa kuchangia bati 300 zenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 8 ili kusaidia kukamilisha ujenzi huo wa mabweni zaidi ya 8 yanayoendelea katika wilaya hiyo
Petel ambaye ni mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya M.M.mechangia bati hizo kama njia ya kuunga mkono jitihada za kunusuru elimu kwa mtoto wa kike wilaya ya Kilolo na uboreshaji wa elimu wilaya hiyo mpya ulioanzishwa na mkuu wa wilaya ya Kilolo Bw Guninita.
Mfanyabiashara huyo ameeleza kuguswa na jitihada hizo zinazofanywa na serikali ya wilaya ya Kilolo kupitia mkuu wa wilaya hiyo katika kumsaidia mtoto wa kike kupata elimu bila kurubuniwa na watu wasiopenda maendeleo ya watoto hao kwa kuwakatisha masomo kwa kuwapa ujauzito.
Hivyo alisema kuwa ili kusaidia ujenzi huo kampuni yake imelazimika kuchangia bati hizo 300 ili kusaidia kuezeka baadhi ya mabweni ambayo ujenzi wake utakuwa umekamilika .
Akikabidhi msaada huo jana kwa mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Kilolo Momahed Gwalima kwa niaba ya mfanyabiashara Patel mkuu wa wilaya ya Kilolo Bw. Guninita alisema kuwa bati hizo 300 zimetolewa na mfanyabiashara huyo baada ya ofisi yake kutuma barua ya maombi kwa mfanyabiashara huyo na wengine .
Guninita alisema kuwa kati ya majukumu aliyonayo katika wilaya hiyo ya Kilolo ni kuhakikisha anasaidiana na wananchi wa wilaya ya Kilolo pamoja na wadau mbali mbali wa maendeleo katika kusukuma mbele gurudumu la maendeleo ya wilaya hiyo ambayo katika mkoa wa Iringa ni wilaya pekee ambayo bado ipo nyuma kwa elimu.
Kwani alisema kuwa mbali ya wilaya hiyo ya Kilolo kuwa ni wilaya ina fursa mbali mbali za kimaendeleo ila bado katika sekta ya elimu hasa katika suala la mabweni ya wanafunzi ,kilolo ipo nyuma na kuwa kupitia mkakati huo ulioanzishwa wa ujenzi wa mabweni na vyumba vya madarasa wilaya hiyo itapiga hatua zaidi katika sekta hiyo ya elimu.
Mkuu huyo wa wilaya alisema kuwa mbali ya wilaya hiyo kuwa na shule zaidi ya 10 za sekondari ila bado wilaya hiyo inachangamoto kubwa ya Hosteli za watoto wa kike na hivyo kuanza ujenzi wa Hosteli katika shule ya sekondari mbali mbali wilayani humo.
Bw Guninita alisema kuwa kwa sasa shule ambazo zitanufaika na msaada huo ni pamoja na sekondari ya Uhambingeto,Gangwa ,Ukwega na Masisiwe na kuwa jitihada zaidi zinaendelea kufanyika ili kuwafikia wadau mbali mbali wa maendeleo katika wilaya hiyo ili kuweza kufanikisha harambee hiyo ya ujenzi wa mabweni na Hosteli katika wilaya ya Kilolo.
Pamoja na kumshukuru mfanyabiashara Petel kwa msaada wake huo wa bati 300 bado alimshukuru mfanyabiashara Asas wa mkoani Iringa kwa kuchangia mifuko ya saruji 200 pamoja na mfanyabiashara Yusuf Manji ambae ni mkurugenzi wa Quality Group kwa kuchangia fedha kiasi cha shilingi 500,000 kwa njia ya hundi kwa ajili ya maendeleo ya elimu wilaya hiyo ya Kilolo na kuwaomba wadau wengine kuendelea kuchangia zaidi.
Kwa upande wake mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Kilolo Bw Ngwalima alimpongeza mkuu huyo wa wilaya kwa jitihada za muda mufupi ambazo amezionyesha katika wilaya hiyo ya Kilolo na kuwa mkuu huyo wa wilaya mbali ya kuwa bado hajapata kumaliza hata mwaka mmoja tangu alipoteuliwa na Rais Jakaya Kikwete ila mambo ambayo amekuwa akiyafanya katika wilaya ya Kilolo ni makubwa na anapaswa kupongezwa kwa utendaji wake kazi.

No comments:
Post a Comment