Naibu Katibu Mkuu Ikulu, Susan Mlawi (wa pili kulia), akiimba pamoja na Kamishna wa Maadili, Jaji mstaafu Salome Kaganda (kulia), wimbo maalum wa maadili, wakati alipowasili kuzindua Tovuti ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, inayopatikana kwa www.ethicssecretariat.go.tz, Ofisi za tume hiyo, jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Jasper Mero kutoka Ofisi ya Taifa Ukaguzi wa Hesabu za Serikali na Mwakilishi wa Jeshi la Polisi Makao Makuu, ACP Patrick Byatao. (Picha zote na Kassim Mbarouk)
Baadhi ya wafanyakazi wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, wakiimba wimbo huo maalum wa maadili, wakati wa uzinduzi wa Tovuti ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, inayopatikana kwa www.ethicssecretariat.go.tz, Dar es Salaam leo.
Baadhi ya wafanyakazi wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, wakiimba wimbo huo, maalum wa Sekretarieti, wakati wa uzinduzi wa Tovuti ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, inayopatikana kwa www.ethicssecretariat.go.tz, Dar es Salaam leo.
Baadhi ya wafanyakazi wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, wakiimba wimbo maalum wa maadili, wakati wa uzinduzi wa Tovuti ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, inayopatikana kwa www.ethicssecretariat.go.tz, Dar es Salaam leo.
Kamishna wa Maadili, Jaji mstaafu Salome Kaganda, akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa tovuti hiyo, Dar es Salaam leo. Kushoto ni mgeni rasmi katika uzinduzi huo, Naibu Katibu Mkuu Ikulu, Susan Mlawi. Tovuti hiyo, inapatikana kwa www.ethicssecretariat.go.tz.
Mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu Ikulu, Susan Mlawi, akizungumza wakati alipokuwa akiizindua tovuti ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, inayopatikana kwa www.ethicssecretariat.go.tz, Ofisi za tume hiyo, Dar es Salaam leo. Kulia ni Kamishna wa Maadili, Jaji mstaafu Salome Kaganda.

Baadhi ya wafanyakazi wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, wakiimsikiliza mgeni rasmi, Naibu Katibu Mkuu Ikulu, Susan Mlawi (hayupo pichani), wakati alipokuwa akizungumza katika uzinduzi wa tovuti hiyo, inayopatikana kwa www.ethicssecretariat.go.tz, Dar es Salaam leo.
Mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu Ikulu, Susan Mlawi (katikati), akizungumza wakati alipokuwa akiizindua tovuti ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, inayopatikana kwa www.ethicssecretariat.go.tz, Ofisi za tume hiyo, Dar es Salaam leo. Kulia ni Kamishna wa Maadili, Jaji mstaafu Salome Kaganda, Jasper Mero (wa kwanza kushoto), kutoka Ofisi ya Taifa Ukaguzi wa Hesabu za Serikali na Mwakilishi wa Jeshi la Polisi Makao Makuu, ACP Patrick Byatao.
Naibu Katibu Mkuu Ikulu, Susan Mlawi, akikata utepe wa kompyuta ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa tovuti ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, inayopatikana kwa www.ethicssecretariat.go.tz, Ofisi za tume hiyo, Dar es Salaam leo. Kushoto ni Kamishna wa Maadili, Jaji mstaafu Salome Kaganda.
Mgeni rasmi katika uzinduzi wa tovuti hiyo, Naibu Katibu Mkuu Ikulu, Susan Mlawi, akikata keki, mara baada ya kuiizindua tovuti ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, inayopatikana kwa www.ethicssecretariat.go.tz, Ofisi za tume hiyo, Dar es Salaam leo. Wa pili kushoto ni Kamishna wa Maadili, Jaji mstaafu Salome Kaganda.
Kamishna wa Maadili, Jaji mstaafu Salome Kaganda (kushoto), akimpa mkono mgeni rasmi katika uzinduzi huo, Naibu Katibu Mkuu Ikulu, Susan Mlawi, mara baada ya kuzindua tovuti ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, inayopatikana kwa www.ethicssecretariat.go.tz, Ofisi za tume hiyo, Dar es Salaam leo.
Mkuu wa Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) wa Sekretarieti hiyo, Masegesa Kamulika, akitoa maelezo mbele ya mgeni rasmi katika uzinduzi huo, Naibu Katibu Mkuu Ikulu, Susan Mlawi (kushoto), kuhusu mambo mbalimbali yaliyomo na yanayopatikana kwenye tovuti hiyo.
Baadhi ya waandishi wa habari, wakifuatilia matukio mbalimbali yaliyokuwa yakitokea katika uzinduzi huo.
Waandishi wa habari, Neema Mngonja (kulia) wa gazeti la Jambo Leo na Khadija Mussa wa gazeti la Uhuru, wakiteta jambo wakati wa uzinduzi wa tovuti hiyo jijini Dar es Salaam leo.
Mgeni rasmi katika uzinduzi wa tovuti hiyo, Naibu Katibu Mkuu Ikulu, Susan Mlawi (katikati aliyekaa), akipigapicha na baadhi ya wakuu wa vitengo vya Sekretariet hiyo, mara baada ya kuzindua tovuti ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, inayopatikana kwa www.ethicssecretariat.go.tz, Ofisi za tume hiyo, Dar es Salaam leo. Kushoto kwake ni Kamishna wa Maadili, Jaji mstaafu Salome Kaganda.
Mgeni rasmi katika uzinduzi wa tovuti hiyo, Naibu Katibu Mkuu Ikulu, Susan Mlawi (katikati aliyekaa), akipigapicha na baadhi ya wafanyakazi wa Sekretariet hiyo, mara baada ya kuzindua tovuti ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, inayopatikana kwa www.ethicssecretariat.go.tz, Ofisi za tume hiyo, Dar es Salaam leo. Kushoto kwake ni Kamishna wa Maadili, Jaji mstaafu Salome Kaganda.

Mgeni rasmi katika uzinduzi wa tovuti hiyo, Naibu Katibu Mkuu Ikulu, Susan Mlawi (katikati), akipigapicha ya kumbukumbu na baadhi ya viongozi wa Sekretariet hiyo na wageni waalikwa mara baada ya kuzindua tovuti ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, inayopatikana kwa www.ethicssecretariat.go.tz, Ofisi za tume hiyo, Dar es Salaam leo. Kushoto kwake ni Kamishna wa Maadili, Jaji mstaafu Salome Kaganda.
Mgeni rasmi katika uzinduzi wa tovuti hiyo, Naibu Katibu Mkuu Ikulu, Susan Mlawi (katikati aliyekaa), akipigapicha na baadhi ya wafanyakazi wa Sekretarieti hiyo wa Kamati ya maandalizi ya uzinduzi wa tovuti ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, inayopatikana kwa www.ethicssecretariat.go.tz, Ofisi za tume hiyo, Dar es Salaam leo. Kushoto kwake ni Kamishna wa Maadili, Jaji mstaafu Salome Kaganda.
Mgeni rasmi katika uzinduzi wa tovuti hiyo, Naibu Katibu Mkuu Ikulu, Susan Mlawi, akiagana na baadhi ya wageni waalikwa kwenye uzinduzi wa tovuti hiyo, ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, inayopatikana kwa www.ethicssecretariat.go.tz, Ofisi za tume hiyo, Dar es Salaam leo, mara baada ya hafla hiyo kumalizika. Kulia ni Kamishna wa Maadili, Jaji mstaafu Salome Kaganda.
Kamishna wa Maadili, Jaji mstaafu Salome Kaganda, akizungumza jambo na wageni waalikwa katika hafla ya uzinduzi wa tovuti hiyo, mara baaa ya kumalizika kwa hafla hiyo, jijini Dar es Salaam leo.
Na Mwandishi wetu
VIONGOZI na Watumishi wa Umma, wametakiwa kuhakikisha wanajaza na kurudisha fomu za tamko la mali na madeni kabla sheria haijachukua mkondo wake.
Agizo hilo lilitolewa leo jijini Dar es Salaam na Kamishna wa Maadili Jaji Salome Kaganda, alipokuwa akizungumza wakati wa uzinduzi wa tovuti ya Sekretarieti ya maadili ya viongozi na watumishi wa umma.
Jaji Kaganda alisema kwamba fomu hizo tayari zimeanza kutolewa kwa wahusika wote na mwisho wa kurudishwa kwake utakuwa Disemba 31 mwaka huu, na kwamba baada ya hapo watakaoukuwa hawajarudisha sheria itachukua mkondo wake.
"Iwapo kiongozi hatochukua fomu kujaza na kurudisha kwa kipindi stahili, atachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria 13 ya mwaka 1995 kwakuwa kukiuka agizo hili ni ukiukaji wa sheria zilizowekwa"alisema Jaji Kaganda.
Alisema kwamba Sekretarieti imeamua kufungua tovuti hiyo ili kuhakikisha kuwa huduma hiyo inawafikia watu wote kwa wakati na kwamba hivi sasa wanaowajibika kujaza fomu hizo wataweza kuzipata kwenye mtandao.
Jaji Kaganda alisema kwamba hatua hiyo itasahidia kuondoa malalamiko ambayo yamekuwa yakitolewa na baadhi ya viongozi walioshindwa kujaza fomu hizo, kwa maelezo ya kutopata fomu hizo kwa urahisi.
Alisema tovuti hiyo itahifadhi taarifa mbalimbali zihusuzo Sekretarieti hiyo, na kwamba watumishi wa umma wanaostahili kujaza fomu hizo wataweza kuzikuta humo.
Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu Ikulu ambaye ndiye alikuwa mgeni rasmi katika uzinduzi huo, alisema uzinduzi wa tovuti hiyo utakuwa imesahidia kupunguza usumbufu wa upatikaji wa fomu hizo.
Alisema kwamba wahusika wanapaswa kuwajibika kuzitafuta fomu hizo kwa haraka kwakuwa upatikanaji wake umerahishwa hili kuhepuka uchukuliwaji wa hatua za sheria.

No comments:
Post a Comment