Mkurugenzi wa kitengo cha huduma za jamii wa Vodafone group, Andrew Dunnet akikagua moja ya mabasi yatakayo tumika kubeba wagonjwa wa Fistula, mabasi hayo yamenunuliwa katika mpango wa kupambana na Fistula uliochini ya CCBRT, Wizara ya Afya na Vodafone uliozinduliwa na Rais Jakaya Kikwete Februali 25.
Mkurugenzi wa kitengo cha huduma za jamii wa Vodafone group, Andrew Dunnet akiwapiga picha kupitia simu yake ya mkononi watoto wanaotibiwa katika Hospitali ya CCBRT Dar es Salaam wakati alipofanya ukaguzi wa wodi za wagonjwa pamoja na Mabasi ya wagonjwa wa Fistula kabla ya kukabidhiwa rasmi kwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr Jakaya Mrisho Kikwete.
Mkurugenzi wa kitengo cha huduma za jamii wa Vodafone group, Andrew Dunnet akifurahi pamoja na watoto wanaotibiwa katika Hospitali ya CCBRT Dar es Salaam wakati alipofanya ukaguzi wa wodi za wagonjwa pamoja na Mabasi ya wagonjwa wa Fistula kabla ya kukabidhiwa rasmi kwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr Jakaya Mrisho Kikwete.
Mwenyekiti wa Bodi ya Hospitali ya walemavu ya CCBRT, Dk. Wilbroad Peter Slaa akimuonyesha maendeleo ya ujenzi Mkurugenzi wa kitengo cha huduma za jamii wa Vodafone group, Andrew Dunnet wakati alipofanya ukaguzi wa wodi za hospitali hiyo kabla ya kukabidhiwa kwa Rais Dk, Jakaya Mrisho Kikwete mapema mwezi huu.
Mwenyekiti wa Bodi ya Hospitali ya walemavu ya CCBRT, Dk. Wilbroad Peter Slaa akimuonyesha maendeleo ya ujenzi Mkurugenzi wa kitengo cha huduma za jamii wa Vodafone group, Andrew Dunnet wakati alipofanya ukaguzi wa wodi za hospitali hiyo kabla ya kukabidhiwa kwa Rais Dk, Jakaya Mrisho Kikwete mapema mwezi huu.
Mkurugenzi wa Kitengo cha huduma wa Vodafone Group, Andrew Dunnet akisikiliza maelezo kuhusu maendeleo ya ujenzi Kutoka kwa Mtaalamu wa Masuala ya Ujenzi wa Hospitali Tom Bourel wakati alipofanya ukaguzi wa ujenzi wa wodi za wagonjwa wa fistula kabla ya kukabidhiwa kwa Dk. Jakaya Kikwete mapema Mwezi huu, Pamoja nao ni Mwenyekiti wa Bodi ya Hospitali ya CCBRT, Dk. Peter Slaa.
Mkurugenzi wa Kitengo cha huduma wa Vodafone Group, Andrew Dunnet akisikiliza maelezo kutoka kwa moja ya wauguzi wa wodi za wagonjwa wa Fistula wa hospitali ya CCBRT, alipofanya ukaguzi wa wodi hizo kabla ya kukabidhiwa kwa Rais, Dr. Jakaya Mrisho Kikwete mapema Mwezi huu. Pamoja nao ni Mwenyekiti wa Bodi ya hospitali hiyo. Dr Wilbroad Peter Slaa.
· Tayari kukabidhiwa kwa Mhe. Rais Dk. Jakaya Kikwete.
· Idadi ya wanawake wanaofanyiwa upasuaji yaongezeka.
Dar es Salaam, 13 Novemba 2012
Mkurugenzi wa Idara ya tiba wa Wizara ya Afya na
Ustawi wa jamii, Dk. Margaret Mhando, Mkurugenzi wa Huduma za Jamii wa
Vodafone group, Andrew Dunnett pamoja na Mwenyekiti wa bodi ya hospitali ya
CCBRT, Dk. Wilbroad Slaa, leo wamefanya ukaguzi wa mradi wa ujenzi wa wodi za
wagonjwa wa fistula pamoja na mabasi matatu ya kubeba wagonjwa katika hospitali
ya walemavu ya CCBRT kabla ya kukabidhiwa rasmi kwa Rais wa Jamuhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt Jakaya Mrisho Kikwete hivi karibuni.
Septemba mwaka 2011, CCBRT na Vodafone Foundation
pamoja na Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii, waliungana kwa pamoja katika
kupambana na magonjwa mbalimbali ya uzazi kwa wanawake ukiwemo ugonjwa wa
fistula ambao umekuwa tishio kwa kinamama wengi hapa nchini. Kampeni hiyo
iliyozinduliwa na Mheshimiwa Rais Jakaya Kikwete tarehe 25 ya mwezi Februali na
kuwezesha upatikanaji wa Dola za kimarekani milioni 10.
Baada ya huduma ya Vodacom M - pesa kuanza
kutumika kutuma fedha za usafiri na matibabu kwa wagonjwa wa Fistula walioko
katika maeneo ya vijijini, kuja CCBRT ili kupata matibabu mpango huo
umeiwezesha hospitali hiyo kutoa matibabu kwa wagonjwa wapatao 1000.
Akizungumzia mpango huo Dk. Janis Perialis ambaye
ni mtaalam wa upasuaji wa ugonjwa wa Fistula amesema kuwa mpango wa kusafirisha
wagonjwa kwa kuwatumia fedha kupitia M - pesa umewezesha hospitali hiyo
kupambana na Ugonjwa wa Fistula kwa kuwafikia wanawake wengi zaidi hasa
wanaoishi maeneo ya vijijini.
“Tunao mabalozi wetu katika mikoa mbalimbali
nchini, wanapopata taarifa kuhusu mwanamke mwenye fistula wanatupa taarifa na
pesa inatumwa kupitia M pesa na wagonjwa wanapofika Dar es salaam hupokelewa na
kuletwa katika hospitali yetu, mpango huo umetuwezesha kupokea wagonjwa kutoka
katika mikoa tofauti nchini na kuwafanyia upasuaji na hatimaye kuwarudisha kwao
wakiwa salama” alisema Perialis.
Mwaka 2014, CCBRT itafungua hospitali mpya ya
huduma za uzazi na watoto itakayotumika
kama rufaa kwa Mkoa wa Dar es Salaam, na kupanua huduma zake kanda ya
mashariki, ili kutoa huduma za uzazi na pia itatumika kama kituo cha mafunzo
kwa wataalam wa afya nchini.
No comments:
Post a Comment