Shughuli za uokozi zilivyoendelea
Juhudi za uokozi katika jengo la ghorofa lililoporomoka wiki jana nchini Ghana zimesitishwa.
Ujenzi mbovu umelaumiwa kwa kuanguka kwa jengo hilo lenye maduka na amblo lilifungua rasmi mapema mwaka huu.
Mmiliki wa jengo hilo, pamoja na afisaa anayesimamia ubora wa majengo, wamezuiliwa.
Rais John Dramani Mahama, alisema kuwa wale waliohusika na kupuuza usalama na ubora wa jengo hilo lazima watachukuliwa hatua kali.
'manusura wangali hospitalini'
Msemaji wa jeshi, kanali, M'bawine Atintande alisema siku ya Jumapili kuwa waokoaji waliweza kufika eneo la chini ya jumba hilo na kwamba hawakuwa na matumaini ya kupata manusura zaidi.
Takriban watu 81 waliokolewa kutoka chini ya vifusi, kumi na wanne kati yao wakiwa wamefariki alisema kanali bila ya kuelezea kwa nini waokoaji walikuwa wamekadiria wale waliofariki kuwa 18.
Kati ya manusura 67 waliopelekwa hospitalini, 13 wangali wanapokea matibabu huku 54 wakiruhusiwa kwenda nyumbani.
Afisaa mmoja alihojiwa na kisha kuachiliwa kwa dhamana.
Mnamo siku ya Alhamisi, idara ya uhandisi nchini humo, ilisema kuwa jengo hilo halikuwa na kibali kumaanisha kuwa huenda halikukaguliwa kabla ya kufunguliwa rasmi
No comments:
Post a Comment