TANGAZO


Monday, November 26, 2012

Rais Kikwete awaapisha Majaji wa Mahakama ya Rufaa, Mjumbe wa Tume ya Uchaguzi, Katibu Tume ya Mabadiliko ya Sheria

Jaji Ibrahim Hamis (kushoto) na Jaji Bethwel Mmila (kulia), wakisubiri kula kiapo katika hafla ya kuwaapisha kuwa Majaji wa Mahakama ya Rufaa, iliyofanyika Ikulu, Dar es Salaam leo, Novemba 26, 2012. (Picha zote na Kassim Mbarouk)
 
Rais Jakaya Kikwete, akimwapisha Jaji Bethwel Mmila kuwa jaji wa Mahakama ya Rufaa Tanzania, katika hafla iliyofanyika Ikulu, Dar es Salaam leo, Novemba 26, 2012.
 
Rais Jakaya Kikwete, akimwapisha Jaji Ibrahim Hamis, kuwa jaji wa Mahakama ya Rufaa Tanzania katika hafla iliyofanyika Ikulu, Dar es Salaam leo, Novemba 26, 2012.
 
Rais Jakaya Kikwete, akimkabidhi vitendeakazi Jaji Ibrahim Hamis, baada ya kumwapisha kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Dar es Salaam leo, Novemba 26, 2012.
 

Jaji Ibrahim Hamis (kushoto) na Jaji Bethwel Mmila (kulia), wakiwa katika picha ya pamoja na Rais Jakaya Kikwete, mara baada ya kuwaapisha kuwa Majaji wa Mahakama ya Rufaa Tanzania, katika hafla iliyofanyika Ikulu Dar es Salaam leo, Novemba 26, 2012.
 
Rais Jakaya Kikwete, akiwa katika picha na Jaji Ibrahim Hamis mara baada ya kumwapisha kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Ikulu Dar es Salaam leo, Novemba 26, 2012.
 
Rais Jakaya Kikwete, akiwa katika ya pamoja na Majaji Ibrahim Hamis (wa pili kushoto) na Bethwel Mmila (kushoto kwa Rais), mara baada ya kuwaapisha kuwa majaji wa Mahakama ya Rufaa, Ikulu Dar es Salaam leo, Novemba 26, 2012.
 
Rais Jakaya Kikwete, akiwa katika ya pamoja na Majaji aliowaapisha Ikulu, Dar es Salaam leo,  Ibrahim Hamis (wa pili kushoto) na Bethwel Mmila (kushoto kwa Rais) pamoja na majaji waliokuwepo katika hafla hiyo.
Jaji John Mkwawa (kulia) na Winfrida Koroso, wakiubiri kuapishwa na Rais Jakaya Kikwete, Jaji Mkwawa kuwa mjumbe wa Tume ya Uchaguzi ya Taifa (NEC) na Koroso kuwa Katibu wa Tume ya Kurekebisha Sheria, Ikulu, Dar es Salaam leo.
 
Rais Jakaya Kikwete, akimwapisha Jaji John Mkwawa kuwa mjumbe wa Tume ya Uchaguzi ya Taifa (NEC) katika hafla iliyofanyika Ikulu, Dar es Salaam leo.
 
Rais Jakaya Kikwete, akimkabidhi vitendeakazi Winfrida Koroso, baada ya kumwapisha kuwa Katibu wa Tume ya Kurekebisha Sheria katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu, Dar es Salaam leo.

Rais Jakaya Kikwete, akiwa katika picha ya pamoja na Jaji John Mkwawa (wa pili kushoto) pamoja na familia yake, mara baada ya kumwapisha kuwa mjumbe wa Tume ya Uchaguzi ya Taifa (NEC), katika hafla iliyofanyika Ikulu, Dar es Salaam leo.
 
Rais Jakaya Kikwete, akiwa katika picha ya pamoja na Winfrida Koroso (wa pili kushoto) pamoja na familia yake, mara baada ya kumwapisha kuwa Katibu wa Tume ya Kurekebisha Sheria katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu, Dar es Salaam leo, Novemba 26, 2012.

No comments:

Post a Comment