TANGAZO


Wednesday, November 14, 2012

Rais Kikwete akutana na Sekretarieti mpya ya CCM Dodoma


 Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa pamoja na Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein (kushoto) pamoja na Makamu Mwenyekiti  mpya wa CCM Bara, Philip Japhet Mangula (kulia), Ikulu ndogo, mjini Dodoma leo. (Picha zote na Freddy Maro)

Mwenyekiti wa CCM, Rais Dk. Jakaya Mrisho Kikwete (wapili kushoto), akizungumza na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Sefu Ali Iddi, Makamu mpya wa CCM Bara, Bwana Philip Mangula (watatu kushoto) pamoja na Makamu wa CCM Bara, aliyemaliza muda wake, Pius Msekwa.

 Mwenyekiti wa CCM, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete, akifurahia jambo pamoja na Makamu Mweyekiti mpya wa CCM Bara, Philip Mangula (katikati) pamoja na Makamu Mwenyekiti wa Bara, aliyemaliza muda wake, Pius Msekwa, Ikulu ndogo mjini Dodoma leo.

 Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Dk. Jakaya Mrisho Kikwete, akiagana na Katibu Mkuu wa CCM aliyemaliza muda wake, Dk. Wilson Mukama, Ikulu ndogo mjini Dodoma leo asubuhi. Dk. Mukama ameteuliwa kuwa Mkuu wa Chuo cha Uongozi  cha CCM.

 Mwenyekiti wa CCM, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Naibu Katibu Mkuu mpya wa CCM, Mwigulu Nchemba Ikulu ndogo mjini Dodoma leo asubuhi.

Mwenyekiti wa CCM, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Katibu mpya wa Oganaizesheni  ya CCM, Mohamed Seif Khatib mjini Dodoma.

No comments:

Post a Comment