TANGAZO


Tuesday, November 20, 2012

NEPAD na COSTECH waandaa mafunzo ya uzalishaji pamba kwa kutumia teknolojia mpya

Naibu Waziri, Ofisi ya Makamu wa Rais, anayeshughulikia mazingira, Charles Kitwanga (katikati), akimsikiliza Mwanasheria wa Ofisi ya Makamu wa Rais, walipokuwa katika mkutano wa mafunzo ya teknolojia ya uhaulishaji wa zao la pamba nchini Bukinafaso hivi karibuni. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Utafiti Costech, Dk. Nicholas  Nyange. Ujumbe huo upo nchini Bukinafaso kwa muda wa siku tano. 
Naibu waziri wa Kilimo na Ushirika, Adamu Malima akijadiliana jambo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Sayansi na Utafiti, Profesa Hassanata Millogo (katikati), ambaye alikuwa mgeni rasimi katika mkutano ambao Serekali ya Tanzania na Wabunge wanahudhuria nchini Bukinafaso, kuhusu jinsi ya uzalishaji wa pamba kwa kutumia teknolojia mpya ya uhaulishaji (BET). Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Ushirikiano wa Maendeleo Afrika (NEPAD), Profesa Diran Makinde. Mkutano huo wa siku tano umeandaliwa na NEPAD na Tume ya Sayansi Tanzania Costech.
 Picha ya pamoja ya ujumbe wa Tanzania na wenyeji wao, nchini Bukinafaso. (Picha zote na Chris Mfinanga)

No comments:

Post a Comment