TANGAZO


Monday, November 19, 2012

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Magesa Mulongo aikaribisha Tume ya Mabadiliko ya Katiba

Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Bw. John Nkolo (aliyesimama) akijitambulisha kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. Magesa Mulongo wakati Wajumbe wa Tume hiyo walipokwenda kujitambulisha kwake jana Jumapili tarehe 18. Novemba, 2012 tayari ya kuanza kazi ya ukusanyaji wa maoni ya wananchi kuhusu Katiba Mpya katika Mkoa huo. Wajumbe wengine ni Bw. Abubakari Ali, Bw. Ussi Ali na Bi. Mwantumu Malale. (Picha zote na Ismail Ngayonga wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba)

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Magesa Mulongo akizungumza na wajumbe wa Tume ya Mabadiliko Katiba jana Jumapili tarehe 18. Novemba, 2012 mara baada ya wajumbe hao kufika ofisini kwake kujitambulisha kabla ya kuanza kazi ya ukusanyaji wa maoni ya wananchi kuhusu Katiba Mpya. Wajumbe hao kutoka kushoto ni Bw. Abubakari Ali, Bw. Ussi Haji na Bi. Mwantumu Malale.

Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Bi. Mwantumu Malale akizungumza wakati wajumbe wa Tume hiyo walipokwenda kujitambulisha kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo jana Jumapili tarehe 18. Novemba, 2012 tayari kuanza kazi ya ukusanyaji wa maoni ya wananchi kuhusu Katiba Mpya mkoani humo. Kulia ni Mkuu wa Mkoa huo, Mhe. Magesa Mulongo.
 
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Magesa Mulongo (wa pili kulia) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba mara baada ya wajumbe hao kujitambulisha kwake jana tarehe 18. Novemba, 2012 tayari kuanza kazi ya ukusanyaji wa maoni ya wananchi kuhusu Katiba Mpya mkoani humo. Kutoka kushoto ni Bw. Abubakari Ali, Bw. Ussi Ali, Bi.  Mwantumu Malale (na wa kwanza kulia) Bw. John Nkolo.

Na Ismail Ngayonga, Arusha
18. Novemba. 2012

MKUU wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo ameihakikishia Tume
ya Mabadiliko ya Katiba mazingira mazuri ya utendaji kazi kwa wakati wote wa kazi ya ukusanyaji wa maoni ya wananchi kuhusu Katiba Mpya Mkoani humo.

Mkuu huyo wa Mkoa aliyasema hayo (jana jumapili tarehe 18.

Novemba,2012) wakati wa mkutano wake na Wajumbe wa Tume
hiyo waliofika Ofisini kwake kwa ajili ya kujitambulisha tayari
kuanza awamu ya nne ya kazi ya ukusanyaji wa maoni ya wananchi
kuhusu Katiba Mpya mkoani humo inayoanza leo jumatatu tarehe
19. Novemba, 2012.

Kwa mujibu wa Mulongo alisema Ofisi yake imejiandaa kikamilifu

kwa ajili ya kazi hiyo na hivyo ipo tayari kutoa msaada  kwa Tume
hiyo pale inapohitaji. “Katika Mikoa ambayo Tume imeitembelea
kazi hii imepita vizuri na sisi tutahakikisha kuwa sifa hiyo na sisi
pia tunaiendeleza” alisema Mkuu huyo wa Mkoa.

Aidha Mulongo alisema Tume hiyo imepewa jukumu kubwa la

kitaifa lenye Baraka za Mhe. Rais na Bunge la Jmahuri ya Muungano wa Tanzania, hivyo ni jukumu la kila mwananchi kuhakikisha kuwa anatoa ushirikiano kwa kadri inavyowezekana.

Kwa upande wake Mjumbe wa Tume hiyo ambaye pia ni Mwenyekiti
wa kundi la Mkoa wa Arusha, Bi. Mwantumu Malale alisema Tume katika imekuwa ikitumia njia mbalimbali za kukusanya maoni ya wananchi wakati  wa mikutano yake ikiwemo njia ya kuzungumza na kuandika.
“Mbali na wananchi pia Viongozi mbalimbali wakiwemo wabunge
nao wamekuwa wakijitokeza kutoa maoni yao kuhusu Katiba Mpya, tunawaomba wananchi wa mkoa wa Arusha nao pia wajitokeze katika mikutano yetu ili nao waweze kutoa maoni yao” alisema Bi. Mwantumu.

Tume ya Mabadiliko ya Katiba leo, Jumatatu tarehe 19. Novemba,

2012 inatarajia kuanza awamu ya nne ya kazi ya ukusanyaji maoni
ya wananchi kuhusu Katiba Mpya katika Mikoa 6 nchini. Mikoa hiyo ni Arusha, Dar es Salaam, Mara, Simiyu, Geita na Mkoa wa Mji Magharibi, Zanzibar.

Mkoani Arusha Tume hiyo leo jumatatu inatarajia kuanza 
kukusanya maoni ya wananchi kuhusu Katiba Mpya katika Wilaya ya Karatu.

No comments:

Post a Comment