Afisa uhusiano wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Bi. Roida Andusamile (wa pili kushoto) akimkaribisha Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE) Bi. Jacqueline Mneney Maleko (wa pili kulia) kugawa vyeti kwa washiriki sambambamba na kufunga Maonyesho ya Vifaa vya Ujenzi na Samani za ndani yaliyofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Kulia ni Meneja Masoko wa Kampuni ya Tanzania Building and Home Improvement EXPO 2012 Bw. Zakaria Malcom ambao ndio waandaaji wa maonesho hayo.
Mshiriki wa maonyesho ya Vifaa vya Ujenzi na Samani za ndani akipokea cheti chake cha ushiriki bora.
Mwakilishi wa Kampuni ya Masoko na Matangazo ya Advent Promotions Nassara Peter akipokea cheti.
Mmoja wa washiriki wa maonesho hayo, akikabidhiwa cheti cha ushiriki wa maonesho ya Sekta ya ujenzi na samani za ndani.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE) Bi. Jacqueline Mneney Maleko, akibadilishana mawazo na baadhi ya washiriki wa maoneysho hayo. Kulia ni Meneja Mauzo Afrika Mashariki wa Kampuni ya Alredha Lighting Bw. Mohammed Mustafa na Katikati ni Mwakilishi wa Kampuni ya Masoko na Matangazo ya Advent Promotions Nassara Peter.

No comments:
Post a Comment