Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara wa Kariakoo (JWK), Mathias Makoi, akizungumza wakati akitoa maelezea mafupi kabla ya kuufungua mkutano huo. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo, Getruda Mamboleo, Makamu Mwenyekiti, Philimon Chonda (wa pili kulia) na Mtunza Fedha, Mwajuma Mbilinyi.
Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo, Getruda Mamboleo, akitoa taarifa katika mkutano huo, kabla ya kumkaribisha Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara wa Kariakoo (JWK), Mathias Makoi (wa pili kushoto), kuufungua mkutano huo, jijini leo. Wa pili kulia ni Makamu Mwenyekiti, Philimon Chonda na Mtunza Fedha, Mwajuma Mbilinyi.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara wa Kariakoo (JWK), Mathias Makoi, akizungumza wakati alipokuwa akiufungua mkutano huo. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo, Getruda Mamboleo na kulia ni Mtunza Fedha, Mwajuma Mbilinyi.
Baadhi ya wajumbe wa mkutano huo, wakipitia ripoti ya Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo, aliyoiwakilisha katika mkutano huo.
Baadhi ya wajumbe wa mkutano huo, wakiipitia ripoti ya Mhazini Mkuu, ikiwemo bajeti ya mwaka ujao ya Jumuiya hiyo.
Kaimu Mhazini Mkuu wa Jumuiya ya Wafanyabiashara wa Kariakoo (JWK), Ombeni Ombeni, akiwasilisha ripoti ya mapato na matumizi kwa mwaka uliopita na bajeti ya mwaka ujao ya Jumuiya hiyo kwenye mkutano huo.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara wa Kariakoo (JWK), Mathias Makoi, akizungumza wakati alipokuwa akiuongoza mkutano huo. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo, Getruda Mamboleo na kulia ni Makamu Mwenyekiti, Philimon Chonda.
Mjumbe wa Jumuiya hiyo, Thomas Kibanga, ambaye alikuwa MC wa mkutano huo, akifafanua jambo kuhusu masuala mbalimbali ya Jumuiya hiyo.
Mjumbe wa Mkutano huo, Petro Mwandemela Kyando, akiwasilisha hoja na mchango wake kuhusu kuiimarisha Jumuiya hiyo.
Makamu Mwenyekiti, Philimon Chonda wa Jumuiya hiyo, akitoa mapendekezo yake juu ya kuimarisha jumuiya hiyo.
Wajumbe wa Mkutano huo, wakisikiliza hoja mbalimbali na michango iliyokuwa ikitolewa kwenye Mkutano Mkuu wa Jumuiya hiyo.
No comments:
Post a Comment