TANGAZO


Friday, November 23, 2012

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahaman Kinana ziarani Geita

 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akikabidhi leseni za wachimbaji wadogo kwenye machimbo ya Mugusu, Geita katika mkutano wa hadhara uliofanyika leo, mkoani Geita. Jumla ya leseni 21 zilikabidhiwa kwa wachimbaji hao baada ya kutolewa na Serikali ili kuwawezesha wachimbaji wadogo nao kunufaika na madini badala ya wachimbaji wakubwa tu.

Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akizindua shina la wakereketwa wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) la wajasiriamali watengeneza fenicha katika mji mdogo wa Katoro mkoani Geita jana. Nape aliwapa pia msaada wa sh. milioni moja kwa ajili ya kuwasaidia wajasiriamali hao kukuza shughuli zao.

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimtuza msanii Kassim Magembe, baada ya kuridhishwa na uhodari wake alipotumbuiza kwenye mkutano wa CCM uliofanyika uwanja wa mpira wa Geita leo.


Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye, akiwasalimia vijana wa kimachinga waliokuwa wakifanyabiashara ya viatu.

No comments:

Post a Comment