TANGAZO


Saturday, November 10, 2012

Jenerali Mstaafu wa JWTZ, George Waitara aupigia kampeni ya kuutaangaza Mlima Kilimanjaro

Mlezi na Mshiriki wa Kupanda Mlima Kilimanjaro, safari ijulikanayo kama 'Annual Kilimanjaro Climb,  Mkuu wa Majeshi mstaafu, Jeneral mstaafu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), George Waitara, akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani), Dar es Salaam leo, kuhusu safari hiyo itakayowashirikisha Wabunge, Wanajeshi na wananchi wa kawaida, ambayo itaanza Disemba 6 na kufika kileleni mwa mlima huo Disemba 9, ambayo ni siku ya  maadhimisho ya Jamhuri na Uhuru wa Tanzania. (Picha zote na Kassim Mbarouk)

Mlezi na Mshiriki wa Kupanda Mlima Kilimanjaro, safari ijulikanayo kama 'Annual Kilimanjaro Climb,  Mkuu wa Majeshi mstaafu, Jeneral mstaafu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), George Waitara, akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, kuhusu safari hiyo itakayowashirikisha Wabunge, Wanajeshi na wananchi wa kawaida, ambayo itaanza Disemba 6 na kufika kileleni mwa mlima huo Disemba 9, ambayo ni siku ya  maadhimisho ya Jamhuri na Uhuru wa Tanzania. Kushoto ni mmoja wa wadhamini wa safari hiyo, Balozi Charles Sanga.

Mmoja wa wadhamini wa safari ya kuupanda Mlima Kilimanjaro, ijulikanayo kwa jina la “ANNUAL KILIMANJARO CLIMB”, Balozi Charles Sanga, akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari kuhusu safari hiyo, itakayoanza Disemba 6 na kufika kileleni Disemba 9 siku ya maadhimisho ya Jamhuri na Uhuru wa Tanganyika. Kulia ni Mlezi na Mshiriki wa Kupanda Mlima Kilimanjaro, Mkuu wa Majeshi mstaafu, Jeneral mstaafu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), George Waitara na kushoto ni Mratibu wa safari hiyo, Joseph Kitani. 

Mlezi na Mshiriki wa Kupanda Mlima Kilimanjaro, safari ijulikanayo kama 'Annual Kilimanjaro Climb,  Mkuu wa Majeshi mstaafu, Jeneral mstaafu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), George Waitara, akijibu baadhi ya maswali ya waandishi wa habari (hawapo pichani), wakati alipokuwa akizungumza nao, kuhusu safari hiyo, itakayowashirikisha Wabunge, Wanajeshi na wananchi wa kawaida, ambayo itaanza Disemba 6 na kufika kileleni mwa mlima huo, Disemba 9, ambayo ni siku ya  maadhimisho ya Jamhuri na Uhuru wa Tanzania. Kushoto ni Mratibu wa safari hiyo, Joseph Kitani na katikati ni mmoja wa wadhamini wa safari hiyo, Balozi Charles Sanga.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU KUPANDA MLIMA KILIMANJARO TAREHE 06 DESEMBA 2012, IJULIKANAYO KAMA “ANNUAL KILIMANJARO CLIMB”
Kampuni ya KJ Traders ikishirikiana na Tanzania Tourist Board (TTB) imeandaa Uhuru expedition ambayo ni mwendelezo wa kumbukumbu ya kutangaza Mlima Kilimanjaro kwa kuwashirikisha watu mbalimbali wakiongozwa na Jenerali Mstaafu George Waitara.

Utaratibu wa expedition hiyo ulianza mwaka 2008 wakati huo ukiratibiwa na M/S KJ Traders na Kibosho Resort, lakini kwa sasa baadhi ya taasisi za Serikali na Mashirika ya Umma nao wameingia na kuleta msisimko mpya kwa nia kukuza utalii kwa kutumia Mlima Kilimanjaro.

Expedition hiyo ya kupanda Mlima inatarajiwa kuanza tarehe 06 Desemba 2012 na kuhitimishwa tarehe 10 Desemba 12, na Waziri wa Maliasili na Utalii atahitimisha rasmi tukio hilo.
Makampuni na Taasisi za Umma ambazo zinatarajia kwa udhamini na ushirika katika tukio hilo ni

o   Tanzania Tourist Board (TTB)

o   Jeshi la Wanachi wa Tanzania

o   Serengeti Breweries Ltd

o   Jeshi la Magereza

o   NMB

o   KJ Traders and General Supplies Ltd

o   Kibosho Resourt

Watu wanaotarjiwa kupanda Mlima safari hii ni Wabunge, baadhi ya wanajeshi na wananchi wa kawaida. Vilevile tunarajiwa kupata Mgeni kutoka nje ya nchi mwanachi wa Tibeti (China).
Kauli mbiu yetu mwaka huu ni “KUKUZA UTALII NA KUTUNZA MAZINGIRA KWA ULINZI SHIRIKISHI”.
Wote mnakaribishwa.
Jenerali Mstaafu George Waitara

No comments:

Post a Comment