Mshindi wa Shindano la Epiq Bongo Star Search 2012 (EBSS), Walter Chilambo akikabidhiwa sanduku lenye kitita cha shilingi milioni 50 baada ya kuibuka mshindi katika shindano hilo lililofanyika usiku wa kuamkia leo kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam. Washindi wengine ni mwanadada Salma Abushiri (Zanzibar), aliyeshika nafasi ya pili na watatu ni Wababa Mtuka wa Dar es Salaam.
Mshindi wa Shindano la Epiq Bongo Star Search 2012 (EBSS), Walter Chilambo, akifurahia zawadi yake baada ya kukabidhiwa usiku wa kuamkia leo, ukumbi wa Diamond Jubillee, Dar es Salaam.
Msanii Barnaba akiimba na mmoja wa washiriki wa shindano la Epiq Bongo Star Search 2012 (EBSS).
|
Mshiriki wa EBSS NshomaNg'hangasamala akiimba moja ya wimbo wake jukwaani.
|
Mwanadada Salma Albushiri akiimba kwa hisia huku akipiga gitaa mbele ya mashabiki wake waliofika kumshuhudia ndani ya ukumbi wa Diamond. |
Mapouda.! majaji hawaishi vituko. (Picha zote kwa hisani ya Habari Mseto na Father Kidevu Blog)
|
No comments:
Post a Comment