TANGAZO


Friday, November 16, 2012

HUAWEI yazindua mpango wa Teknohama katika Sekta ya Elimu nchini



Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Profesa Makame Mbarawa, akizungumza na wageni waalikwa wakati wa uzinduzi wa mpango kabambe wa Teknohama katika Sekta ya Elimu nchini ,uliofadhiliwa na Kampuni ya HUAWEI kutoka China jijini Dar es Salaam leo.
Katika mradi huo, wa Teknohama itayowezesha Watanzania mbalimbali kutoka shule za Sekondari na Vyuo, kupata vifaa na mafunzo ya Sayansi na Teknolojia ili kusukuma mbele maendeleo katika nyanja za Uchumi na Kijamii.
 
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya HUAWEI kutoka China, Bruce Zhang akizungumza katika hafla hiyo, kwamba Mpango huo, unaoitwa “Huawei ICT Star”, itasaidia katika shule za Msingi na Sekondari katika kusukuma mbele maendeleo ya Sayansi na Teknolojia nchini Tanzania. Alisema katika Program hii itasaidia kuboresha miundombinu katika Sanyansi na Teknolojia ili kutoa mwamko kwa vijana wa Kitanzania kujifunza masomo ya Sayansi na Teknolojia.


Balozi wa China nchini Tanzania, Lu Youqing, akitoa maelezo yake, wakati wa uzinduzi wa mpango wa Teknohama katika Shule na vyuo nchini Tanzania. Balozi Youqing, alisema mpango huo ni mwendelezo wa uhusiano mwema kati ya Tanzania na Jamhuri ya watu wa China katika nyanja mbalimbali za biashara, Uchumi na Kijamii. Aliongeza kwamba Serikali ya China itaendelea na mikakati yake ya kusaidia nchi ya Tanzania ili kuweza kufikia malengo ya Milenia ya 2015.
 
Viongozi wakiwa meza kuu wakati wa mkutano huo.
 

Mgeni rasmi, Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Profesa Makame Mbarawa (wa pili kushoto) na Balozi wa China, Lu Youqing (wa tatu kulia), wakizindua rasmi mpango wa “HUAWEI ICT STAR” nchini Tanzania jijini Dar es Salaam leo.


Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Profesa Mbarawa na Mkurugenzi Mtendaji wa HUAWEI, Bruce Zhang wakitiliana saini kitabu cha makubaliano rasmi ya Ushirikiano katika Sekta ya Sayansi na Teknolojia kupitia Elimu.
 

Waziri Profesa Mbarawa (kushoto), akikabidhi zawadi kwa Mkurugenzi Mtendaji wa HUAWEI, Bruce Zhang.
 
Baadhi ya wageni waalikwa waliohudhuria uzinduzi huo, wakifuatilia matukio mbalimbali yaliyokuwa yakitendeka ukumbini humo.
 
Baadhi ya wageni waalikwa waliohudhuria uzinduzi huo, wakifuatilia matukio mbalimbali yaliyokuwa yakitendeka ukumbini humo.
 

Mgeni rasmi, Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Profesa Makame Mbarawa, akiondoka ukumbi baada ya uzinduzi huo. (Picha zote na John Bukuku wa Fullshangwe)

No comments:

Post a Comment