TANGAZO


Friday, November 16, 2012

Mtoto Aneth aliyeunguzwa na maji ya moto aendelea vizuri baada ya kukatwa mkono wa kushoto uliounguzwa

 

Mtoto Anetha akiwa anaendelea vizuri baada ya kukatwa mkono wake wa kushoto jana, uliounguzwa kwa maji ya moto na mama yake mdogo.
ANETH akitayarishiwa chakula na mama yake mdogo, Slivia, anayemhudumia hospitalini hapo. 
Kiujumla mtoto ANETH sasa anaendelea vizuri na sasa anaweza kula chakula vizuri. Pia taarifa zinadai kwamba mama yake mzazi yupo njiani kuelekea Mbeya, akitokea Kagera kupitia Dar es Salaam.

HALI ya Mtoto Aneth Johanes (4) aliyelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mbeya kufuatia kuchomwa moto mkono wake wa kushoto na anayedaiwa kuwa ni Shangazi yake inaendelea vizuri licha ya kufanyiwa upasuaji uliolazimu kukatwa kwa mkono huo.
Kwa mujibu wa mama mdogo wa mgonjwa anayemhudumia hospitalini hapo Silvia Salvatory alithibitisha kuendelea vizuri kwa motto huyo ambapo alisema ilimlazimu kufanyiwa upasuaji kutokana na mkono huo kukosa mawasiliano na kuonekana kuvunjika.
Alisema taarifa za awali zinaonesha shangazi yake huyo Bahati Rukangara alianza kumtesa mtoto huyo muda mrefu mara baada ya kumchukua kutoka kwa wazazi wake wanaoishi Bukoba Mkoani Kagera.
Aliongeza kuwa tangu amchukue kwa wazazi wake Februari Mwaka huu amewahi kumjeruhi mkono wake wa Kulia hadi kuuvunja ambapo hadi sasa mtoto huyo alikuwa akitegemea mkono wa kulia ambao nao umekatwa.
Tukio hilo la kisikitisha lilitokea juzi majira ya saa nne asubuhi baada ya majirani kusikia yowe la mtoto huyo akiomba msaada kutokana na mateso na maumivu makali aliyokuwa akiyapata kutokana na adhabu hiyo kutoka kwa Shangazi yake
.
Muuguzi mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Mbeya Thomas Isidori alisema hali iliyopelekea kukatwa kwa mkono wa mtoto huyo ni siri kati yake na daktari aliyemhudumia na kwamba sheria ya uuguzi inakataza kutoa taarifa ambazo ni siri.
Isidori alipoulizwa sababu za mgonjwa huyo kufanyiwa upasuaji mapema mno hadi kusababisha ulemavu alisema ni suala la kitaalamu ambalo hata yeye hawezi kulijibu na ni sheria ambayo inawataka madaktari kutunza siri za wagonjwa.
Hata hivyo muuguzi huyo alizuia kabisa waandishi wa habari kupiga picha za motto huyo baada ya kufanyiwa upasuaji huo uliosababisha kukatwa mkono kwa mgonjwa huyo.
Baadhi ya wananchi waliofika Hospitalini hapo kumjulia hali mtoto Aneth aliyelazwa Wodi namba Nane ambao hawakutaka kutaja majina yao walilaani kitendo cha madaktari kukimbilia kukata mkono mgonjwa badala ya kujaribu njia zingine za kunusuru hali hiyo.

No comments:

Post a Comment