TANGAZO


Wednesday, November 14, 2012

Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (NEC-CCM), yakutana mjini Dodoma leo

 

KIKAO cha Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (NEC-CCM), kimekutana katika ukumbi wa mikutano wa Makao Makuu ya chama, maarufu kama White House, mjini Dodoma leo,  tarehe 14th Nov 2012  

Kikao hicho kitajadili juu ya kuunda na kupitisha majina yaliyopendekezwa  na Mwenyekiti wa Chama Mapinduzi Mheshimiwa Dk. Jakaya Mrisho Kikwete,  ya wajumbe wa Kamati Kuu ya Chama ya Taifa (CC) pamoja na uundaji wa Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya Taifa.

Mwenyekiti wa Chama kwa mujibu wa Kanuni na Katiba ya Chama Cha Mapinduzi, anayo fursa ya kuteua wajumbe kumi(10) wa Halmashauri Kuu ya Taifa, ambapo  Mwenyekiti aliwateua wajumbe wanne(4) na akabakiza nafasi nyingine sita.  Miongoni mwa wajumbe hao ni Mhe. Asha-rose Migiro, Mhe. Zakhia Meghji, Mhe. Nape Nnauye na  Mhe. Abdulrahaman Kinana.

     Baada ya uteuzi huo, Mwenyekiti pia alipendekeza majina ya wajumbe wa Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya Taifa, ambapo alipendekeza majina yafuatayo;
  1. Nafasi ya Katibu Mkuu, alimpendekeza Mhe. Abdulrahaman Kinana.
  2. Nafasi ya Naibu Katibu Mkuu Zanzibar,  Mhe. Vuai Ali Vuai.
  3. Nafasi ya Naibu Katibu Mkuu Bara, Mhe. Lameck Madelu Nchemba.
  4. Katibu wa Oganaizesheni ni Ndugu Mohamed Seif Khatibu.
  5. Katibu wa Siasa na Mahusiano ya Kimataifa, Asha-rose Migiro.
  6. Katibu wa Uchumi na Fedha, Zakhia A. Meghji.
    Baada ya mapendekezo hayo, Halmashauri Kuu ya Taifa, ilipitisha majina hayo na kuyakubali kuwa hao waliopendekezwa ndio hasa wanaofaa kuwa wajumbe wa Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya Taifa.




Pia, Mwenyekiti akawashukuru wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa waliopita na pia kuwataka wajumbe wapya kuchapa kazi na kuwataka kujenga mustakabali wa Chama, Uimara na Umadhubuti kwa kufanya kazi kwa kushirikiana na kusaidiana.


Abdulrahman Kinana-Katibu Mkuu wa CCM, Taifa


 Mwigulu Nchemba-Naibu Katibu Mkuu, Bara

 























Vuai Ali Vuai - Naibu Katibu Mkuu, Zanzibar


 
























Nape Nnauye-Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi.



  























Asha-Rose Migiro- Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa.





Zakia Meghji-Katibu wa NEC, Uchumi na Fedha

Muhamed Seif Khatib, Katibu wa NEC, Oganaizesheni



 

No comments:

Post a Comment