Ameongeza
kuwa Wiki ya Umoja wa Mataifa kwa mwaka 2012 inaadhimishwa kwa shughuli
mbalimbali zinazolenga vijana, wanafunzi, wasomi, vyombo vya habari na jamii kwa
ujumla.
Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia na kuandika habari zilizokuwa zikitolewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje, Dar es Salaam leo/. |
Katibu Mkuu
wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bw. John Haule
akizungumzia maadhimisho ya miaka 67 ya Umoja wa Mataifa ambapo pamoja na mambo
mengine amesema kutakuwa na maonyesho yatakayofanyika katika viwanja vya
Karimjee siku ya tarehe 23 na 24 mwezi huu ambapo wananchi wataona mipango na
miradi mbalimbali ambayo Umoja wa mataifa umekuwa ukiisaidia Tanzania na pia
amesema kutakuwa na mjadala wa wazi katika ukumbi huo siku ya tarehe 23 ambapo
wananchi wanakaribishwa kushiriki na kutoa mawazo yao.
Na Mwandishi
wetu
Tanzania
inaungana na nchi nyingine mbalimbali duniani kuadhimisha miaka 67 ya Umoja wa
Mataifa ambapo kutakuwa na shughuli mbali mbali zinazoanza leo tarehe 17 mpaka
siku ya tarehe 24 Oktoba ambayo ndio siku ya kilele cha shughuli
hizo.
Kitaifa
nchini Tanzania miaka 67 ya Umoja wa Mataifa itaadhimishwa kwa kauli mbiu ambazo
zimekuwa zikitoka kila mwaka na kauli mbiu ya mwaka huu ni ‘Changing Peoples’
Lives: Greening The Environment For Sustainable
Livelihoods’.
Akizungumza
na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo
ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bw. John Haule amesema kauli mbiu hiyo
imekuja wakati muafaka ili kutukumbusha mahusiano yetu ndani ya Jumuiya ya Umoja
wa Mataifa lakini vilevile inatukumbusha changamoto ya jinsi uharibifu wa
mazingira unavyofanyika hivi sasa. Ameongeza kuwa wiki ya
maadhimisho ya miaka 67 ya Umoja wa Mataifa itaadhimishwa na matukio mbali mbali
ikiwemo uzinduzi wa leo, na Siku ya Familia itakayohusisha michezo mbali mbali
itakayofanyika kwenye viwanja wa Leaders Club tarehe 20 Oktoba
2012.
Michezo hiyo
itawahusisha wanadiplomasia waliopo nchini Tanzania, wafanyakazi wa Umoja wa
Mataifa na wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje.
No comments:
Post a Comment