TANGAZO


Saturday, September 15, 2012

Ziara ya Waziri Mkuu Pinda Ngudu


Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, akifungua mradi ya Ufugaji nyuki katika kijiji cha  Nkalalo, wilayani Kwimba akiwa katika ziara ya Mkoa wa Mwanza Septemba 14, 2012. Nyuma yake ni mkewe, Tunu na kushoto kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhandisi Evarest Ndikilo na Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Kwimba, Suleiman Mzee. 
Wasanii wa Kikundi cha Ng’wanadelema cha Ngudu, wilayani Kwimba, wakicheza ngoma ya Wayeye wakati Waziri Mkuu, Mizengo Pinda alipowasalimia wananchi katika kijiji cha Nkalalo, wilayani Kwimba, akiwa katika ziara ya Mkoa wa Mwanza Septemba 14, 2012. 
 
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na mkewe Tunu, wakiwa wamevikwa mavazi ya kiongozi wa jadi wa Sungusungu katika mkutano wa hadhara uliohutubiwa na Waziri Mkuu kwenye uwanja wa mpira wa miguu wa Ngudu, Septemba 14, 2012.
Baadhi ya Wananchi wa Wilaya ya Kwimba, wakimsikiliza Waziri Mkuu, Mizengo Pinda wakati alipohutubia katika mkutano wa hadhara uliofanyika uwanja wa mpira wa miguu  wa Ngudu, akiwa katika ziara ya Mkoa wa Mwanza, Septemba 14,2012. (Picha zote na Ofisi ya Waziri Mkuu)

No comments:

Post a Comment