Mke wa Rais, Mama Salma Kikwete (katikati), akicheza ngoma ya Segere wakati wa sherehe iliyoandaliwa na Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT-CCM), kumkaribisha na kumpongeza, aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), Dk. Asha Rose Migiro (kushoto) kwa kuwa mwamamke wa kwanza Afrika kushika wadhifa huo. Hafla hiyo, imefanyika leo viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam. (Picha zote na Richard Mwaikenda)
Spika wa Bunge, Anne Makinda (kushoto) na Mama Maria Nyerere, wakiangalia wanawake wakiserebuka na muziki wakati wa sherehe hizo.
Aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), Dk. Asha-Rose Migiro (aliyevaa kilemba kushoto), akijumuika kucheza segere wakati wa sherehe, iliyoandaliwa na Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT-CCM), kumkaribisha na kumpongeza kwa kuwa mwamamke wa kwanza Afrika, kushika wadhifa huo, leo kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam.
Mama Migiro akiwapungia wageni mbalimbali na wananchi, mashabiki wa Chama hicho katika sherehe hizo.
No comments:
Post a Comment