Akivalishwa taji lake la Redd’s Miss Kinondoni 2012.
Mshindi wa shindano la Redds Miss Kinondoni Brigiter Alfred, akiwapungia mkono mashabiki walioshuhudia shindano hilo jijini Dar es Salaam jana, kulia ni mshindi wa pili Diana Hussein na mshindi wa tatu Irene David. Brigit pia anashikilia taji la Redds Miss Sinza 2012 huku Irene akishikilia taji la Miss Ubungo 2012. Pamoja na hayo Redd’s Miss Kinondoni 2012 alijishindia taji la Miss Talent iliyokuwa umedhaminiwa na Perfect Lady Classic Saloon iliyopo Kinondoni jijini Dar na wamempa zawadi ya kupewa huduma kwa kipindi cha mwaka mzima
ndani ya Saloon yao.
Tano bora wa Redd’s Miss Kinondoni 2012.
Huyu, amejinyakulia kuwa Balozi wa Mwananyamala katika shindano hilo la Redd’d Miss Kinondoni 2012, ambaye kazi yake kubwa itakuwa ni katika kuhamasisha kuchangia mfuko wa akina mama.
Warembo walioshiriki shindano hilo wakiwa kwenye vazi la ufukweni mbele ya majaji na mashabiki wa shindano hilo lililofanyika jijini Dar es Salaam usiku wa jana. Hii sio kiduku ni midundo ya kihindi mshiriki wa shindano hilo Brigit Alfred, akionyesha uwezo wake kwenye kucheza na kuibuka kidedea kwenye kipaji lakini pia aliibuka kidedea kwenye shindano hilo na kuwa Miss Kinondoni 2012. Mshindi tatu kwenye shindano hilo Irene David akiwa kwenye vazi la jioni.
Hawa ndio washiriki waliofika tano bora kutoka kushoto ni, Judith Sangu, Brigit Alfred, Diana George Hussein, Irene David na Kudra Lupatu.
Mshindi wa shindano hilo Brigit Alfred akipunga mkono mara baada ya kutangazwa kuwa mshindi wa shindano hilo.Mshindi wapili kwenye Shindano hilo Diana George Hussein akiwa kwenye vazi la jioni.
No comments:
Post a Comment