TANGAZO


Monday, September 17, 2012

Ziara ya Waziri Mkuu Pinda Ilemela mkoani Mwanza



Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na mmoja wa wageni katika harambe ya kuchangia ujenzi wa Kanisa Katoliki la Pansiasi wilayani Ilemela Septemba 16, 2012. Zaidi ya Shilingi milioni 70, zilichangwa katika harambee hiyo.

Mke wa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, Tunu Pinda, akimshukuru Mbunge wa zamani wa Busega, Raphael Chegeni ambaye alichangia shilingi milioni moja katika harambe ya kuchangia ujenzi wa Kanisa Katoliki la Pansiasi wilayani Ilemela Septemba 16, 2012. Zaidi ya Shilingi milioni 70, zilichangwa katika harambee hiyo. 
 
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, akisalimiana na mafundi na wahandisi  wa Kampuni ya ujenzi wa barabara ya  Nyaza Road  inayojenga kwa kiwango cha lami barabara  ya Pansiasi Buzuruga wakati alipoweka jiwe la misngi la ujenzi wa barabara hiyo, akiwa katika ziara ya mkoa wa Mwanza jana, Septemba 16, 2012.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Wasanii wa kikundi cha sanaa cha Bujora, wilayani Ilemela, wakicheza ngoma ya Bugobogobo, wakati Waziri Mkuu Mizengo Pinda, alipohutubia mkutano wa hadhara  kwenye uwanja wa Mgomeni, Kirumba akiwa katika ziara ya Mkoa wa Mwanza, jana Septemba 16, 2012. (Picha zote na Ofisi a Waziri Mkuu)

No comments:

Post a Comment