TANGAZO


Monday, September 17, 2012

Waziri Nchimbi azindua Wiki ya Nenda kwa Usalama barabarani mkoani Iringa



Waziri wa mambo ya ndani, Dk. Emmanuel Nchimbi akitoa hotuba yake wakati wa uzinduzi wa Wiki ya Nenda kwa usalama barabarani, Uwanja wa Samora mjini Iringa leo. Viongozi mbalimbali wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani na Mabaraza mbalimbali kutoka Mikoa na Wilaya, walihudhuria katika muzinduzi huo.
Waziri wa mambo ya Ndani, Dk Emmanuel Nchimbi, akipokea Mordem ya Airtel kutoka kwa Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Airtel, Jackson Mbando wakati alipotembelea banda la kampuni hiyo katika uzinduzi wa wiki ya nenda kwa usalama barabarani, mjini Iringa leo. Wa pili kutoka kulia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Silima Pereira na Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Dk. Christine Ishengoma.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani  na Mwenyekiti wa Baraza la Usalama barabarani Taifa, Silima Pereira, akisoma hotuba yake wakati wa uzinduzi wa wiki ya Usalama barabarani mkoani Iringa leo.
Wanafunzi wa Shule mbalimbali za Msingi, wakiwa wamekaa wakiangalia matukio mbalimbali yaliyokuwa yakijiri katika uzinduzi huo.

Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk. Emmanuel Nchimbi akimkabidhi cheti, Beda Meneja wa Airtel Kanda ya Nyanda za Juu Kusini kutokana na mchango wa kampuni hiyo katika maadhimisho hayo.
Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Dk. Cheristine Ishengoma, akitoa hotuba yake, mbele ya Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk. Emmanuel Nchimbi (wa pili kulia), wakati akiwasilisha salama za Mkoa wake huo, katika maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa usalama barabarani uwanja wa Samora mjini Iringa leo.
Viongozi mbalimbali wa Mabaraza ya Usalama Barabarani na mgeni rasmi, wakiwa kwenye meza kuu wakifuatilia matukio mbalimbali yaliyokuwa yakitendeka katika uzinduzi huo.

Pilisi wakiwa kwenye banda leo kwenye maonesho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama, mjini Iringa leo. 

Brasi Bendi ikiyoongoza maandamano hayo ya Wiki ya Nenda kwa Usalama leo.
Mwenyekiti wa Baraza la Usalama Barabarani, mkoani Iringa, Salim Ahmed akisalimiana na Mwenyekiti wa Baraza la Usalama barabarani Taifa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Silima Pereira wakati alipowasili katika uwanja wa Samora.
Maafisa mbalimbali wa Kikosi cha Usalama barabarani kutoka Makao Makuu wakiwa  kwenye maadhimisho hayo, mjini Iringa leo. 
Waziri wa Mambo ya Ndani  ya Nchi, Emmanuel Nchimbi, akisalimiana na Mwenyekiti wa Baraza la Usalama Barabarani, mkoani Iringa mara baada ya kuwasili katika uzinduzi huo, uwanja wa Samora, mjini Iringa leo.
Kutoka kulia ni  Theresia Kimaro Mkaguzi wa Polisi kutoka Makao Makuu ya Trafiki, Inspekta Sauda Mohamed, Inspekta Kulthum Bambo na Inspekta Agatha Isaack wakiwa katika maadhimisha hayo, mkoani Iringa leo.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Silima Pereira akipita katika banda la Polisi wakati wa uzinduzi wa Wiki ya Nenda kwa Usalama leo, mjini Iringa. Aliyeongozana naye ni Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohamed Mpinga.
Waziri wa Mambo ya ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi akipata maelezo kutoka katika banda la Polisi kwa Ispekta Abel Bartazar Swai. Kulia ni Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohamed Mpinga.
Askari wa Kikosi cha Zimamoto, akimuokoa mmoja wa majeruhi wa mfano katika ajali, baada ya kufanikiwa kukata milango ya gari na vifaa maalum ambamo majeruhi huyo, alikuwa amenaswa na vyuma.
Mmoja wa wasanii wa Kikundi Mizengwe, akiigiza kama trafiki katika maadhimisho hayo.
Meneja Masoko wa kiwanda  cha maziwa cha ASAS DAIRIERS LTD cha Iringa, Ahmed Omary Kasu, akimpa maelezo Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Silima Pereira, wakati alipotembelea katika banda hilo na kuona shughuli zao.
Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk. Emmanuel Nchimbi, akisikiliza maelezo kutoka kwa Ofisa Uhusiano wa SUMATRA, David Mziray wakati alipotembelea katika banda hilo, katika maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa usalama Barabarani, mjini Iringa leo. Katikati ni Kaimu Mkurugenzi wa SUMATRA, Ahmad Kilima. (Picha zote na John Bukuku, Iringa)

No comments:

Post a Comment