TANGAZO


Wednesday, September 19, 2012

Waziri Mwinyi atembelea Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), jijini Dar



Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Emanuel Humba akitoa maelezo ya moja ya miradi ya Mfuko huo kwa Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Hussein Mwinyi.
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Hussein Mwinyi akizungumza na wafanyakazi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, alipofanya ziara Makao Makuu ya mfuko huo, leo.
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Hussein Mwinyi akitoa maelekezo kwa viongozi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya kuhusiana huduma zitolewazo na mfuko huo.
Wafanyakazi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya wakimsikiliza, Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Hussein Mwinyi, alipofika kwa lengo la kuzungumza nao, Makao Makuu ya Mfuko huo, jijini Dar es Salaam leo.
Baadhi ya Wajumbe wa Bodi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (walioko mbele) wakisikiliza kwa makini maelekezo ya Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Hussein Mwinyi, wakati alipotembelea Makao Makuu ya mfuko huo, jijini leo. (Picha zote na mdau wetu)

No comments:

Post a Comment