Waziri Mkuu Pinda, ziarani Ukerewe
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na mkewe, Tunu (kushoto), wakivuka kwa Pantoni la MV. Ujenzi, kutoka Kisorya hadi Rugezi, Ukerewe wakiwa katika ziara ya Mkoa wa Mwanza Septemba 11, 2012. Aliyekaa kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhandisi Evarest Ndikilo na kushoto kwake ni Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Mwanza, Clement Mabina.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, akisalimiana na Viongozi wa Wilaya ya Ukerewe baada ya kuwasili Mjini Nansio kwa ziara ya kikazi juzi, Septemba 11, 2012. Kushoto ni Mkuu wa WIlaya hiyo, Mary Tesha.
Wasanii wakitumbuiza wakati Waziri Mkuu, Mizengo Pinda alipohutubia mkutano wa hadhara kwenye Uwanja wa Getreude Mongella, mjini Nansio, akiwa katika ziara ya Mkoa wa Mwanza, juzi Septemba 11, 2012.
Wananchi wakivuka kwa kutmia mtumbwi kwenda kwenye mkutano uliokuwa ukihutubiwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, wakati wa ziara yake ya Mkoa wa Mwanza juzi, Septemba 11, 2012. (Picha zote na Ofisi ya Waziri Mkuu)
No comments:
Post a Comment