Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Six Telecoms, Rashid Shamte, akifafanua jambo kuhusiana na Mkutano Mkuu wa wafanyabiashara wakubwa duniani wa masuala ya mawasiliano, ujulikanao kwa jina la Capacity Africa unaoanza kesho kwenye Hotel ya Hyatt Regency ya jijini. Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Profesa Makame Mbarawa ataufungua mkutano huo.
DAR ES SALAAM, Tanzania
MKUTANO wa Sita wa wafanyabiashara wakubwa wa watoaji huduma za mtandao wa internet, simu za mikononi, ujilikanao kwa jina la Capacity Africa, utafanyika kwa mara ya kwanza nchini Tanzania kuanzia Septemba 13 mpaka 14 kwenye Hotel ya Hyatt Regency ya jijini.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Six Telecoms Company Limited, ambao ni wadhamini wakuu Mkutano huo, Rashid Shamte, mkutano wa mwaka utawashirikisha wafanyabiashara wakubwa 380 na watoa huduma 150 kutoka nchi 50 za bara la Afrika.
Mkutano wa Capacity Africa umekuwa nyenzo muhimu sana kwa maendeleo ya bara la hili katika kuanzisha ushirikiano wa kibiashara na wafanyabiashara mbalimbali hasa kwa watoa huduma ya biashara ya katika sekta ya mawasiliano.
Miaka iliyopita, mkutano huo ulifanyika mjini Cape Town , Afrika Kusini na Nairobi , Kenya na ni heshima kubwa kwa Tanzania kupata fursa ya kuandaa mkutano huu.
Shamte alisema kuwa Kampuni yake imefanya kazi kubwa kuuwezesha mkutano huo kufanyika hapa nchini na hii inatokana na jinsi inavyotoa huduma hiyo kwa njia ya mkondo wa kisasa wa majini kwa nchi za Afrika Mashariki katika miji ya Dar es salaam Tanzania , Nairobi Kenyana Kampala Uganda .
Alisema kuwa kampuni yake pia inatoa huduma hiyo katika miji mingine mikubwa duniani kama London , Paris , New York ,Dubai na Johannesburg .
Alifafanua kuwa , kampuni ya Six Telecoms inaheshimika zaidi ya wafanyabiashara wajulikanao kwa jina la 260 Teir-1 duniani kwa kutoa huduma bora ya sauti, data na huduma ya ziada katika nchi zilizopo za ukanda wa Sub –Sahara za Afrika na za kimataifa.
“Kampuni yetu ni ya kwanza kwa utoaji wa huduma ya mitandao ya internet, simu, sauti na huduma ya data kwa nchi za Afrika Mashariki na sababu hiyo imewafanya wao kuhakikisha mkutano huu unafanyika nchini na kuchukua udhamini mkuu.
Shamte ambaye atakuwa mmoja wa watoa mada wakuu katika mkutano huo alisema kuwa ni fursa kwa wadau wa biasharayao kushiriki katika mkutano huo ili kufikia malengo yao ya kibiashara.
Mkutano huo wa siku mbili utakuwa wa mahojiano, uwasilishwaji wa mada mbalimabli, majadiliano pamoja na maonyesho ya jinsi ya utoaji wa huduma hiyo.
Wadhamini wengine wa mkutano huu ni Liquid Telecom, WIOCC, Safaricom Business, Seacom, Gateway n.k
No comments:
Post a Comment