Mkuu wa Itifaki wa Miss Tanzania, Albert Makoye, akifungua mashindano ya Redd’s Miss Kinondoni Talent. Kulia ni Ssebo ambaye ni mmoja wa wajumbe wa bodi wa Redd’s Miss Kinondoni 2012, ambaye alikuwa mshereheshaji katika shindano hilo, lililofanyika Hoteli ya JB Belmonte, iliyopo jengo la Benjamin Mkapa, Dar es Salaam. Mashindano hayo yalidhaminiwa na Perfect Lady Classic Saloon iliyopo Kinondoni jijini Dar na wametoa zawadi kwa washindi watatu waliopatikana kwa kupewa huduma kwa kipindi cha mwaka mzima ndani ya Saloon yao. Shindano rasmi la kumsaka Redd’s Miss Kinondoni linatarajiwa kufanyika Ijumaa tarehe Septemba 14, 2012 katika Ukumbi wa Cassa Complex uliopo Mikocheni jijini.
Mmoja wa warembo hao, akionesha kipaji chake kwenye shindano hilo. |
Mshiriki namba 3, Nahma Saidi akikata mauno kwa kucheza ngoma za mambo ya Pwani.
Mshiriki namba 2, Ester Musa alionyesha kipaji cha kuimba.
Mshiriki namba 1, akionyesha umahiri wake wa kukata mauno.
Mshiriki namba 4, Diana Hussein akionyesha kipaji cha kubuni mavazi.
Brigitter Alfred, mshiriki namba 9, akionesha umahili wake wa kuimba na kucheza ngoma za kihindi.
Majaji wa shindano la Redd’s Miss Kinondoni Talent, Man Maji (kulia) na mwanadada wakifuatilia kwa makini.
Mshiriki namba 10, Kudra Lupatu akionesha kipaji cha kubuni mavazi kwa staili ya kumvalisha mshiriki mwenzake.
Kudra Lupati katika pozi mara baada ya kumaliza kutambulisha vazi lake.
Mshiriki wa Redd’s Miss Kinondoni, akichora picha ya mlima Kilimanjaro.
Ssebo, mmoja wa wanabodi ya Redd’s Miss Kinondoni 2012, alikuwa mshereheshaji wa shindano hilo la Talent, akimkaribisha Mratibu wa Redd’s Miss Kinondoni 2012, Vivien Sirikwa (kulia), kuongea machache.
Mkurugenzi wa Perfect Lady Classic Saloon, Ester Kiama ambao ndiyo waliokuwa wamedhamini Redd’s Miss Kinondoni Talent, akitangaza zawadi alizowapatia warembo walioshinda.
Wakiwa katika nyuso za furaha ni warembo walioshinda katika Kinyang’anyiro cha Redd’s Miss Kinondoni Talent kutoka kulia ni Judith Sangu, Brigitter Alfred na Diana Hussein. Warembo hao wamepatiwa zawadi ya kupewa huduma Perfect Lady Saloon kwa kila mmoja kipindi cha Mwaka mzima.
Warembo wakiserebuka mara baada ya shindano hilo kuishi.
Hapa ni ngoma tu, warembo wakiserebuka kwa ngoma za shoo, zilizokuwa zikimwagwa kwenye ukumbi huo, wakati wa shindano hilo. |
Mpaka chini, serebuka ee, mpaka chini, macho juu mama wee macho juu... |
…Hapa ni mwendo wa Kwaito…
Muziki umenoga kwa mwalimu na mwanafunzi.
Ssebo ambaye ni mmoja kati ya mwanabodi wa Redd’s Miss Kinondoni 2012 na alikuwa ni mshereheshaji katika shindano hilo la Talent akiongea machache na Mkurugenzi wa Perfect Lady Saloon, Ester Kiama.
Shoo Love nayo ilikuwepo kwa muaandaji na mdhamini.
No comments:
Post a Comment