Rais Jakaya Kikwete katika ziara ya Kiserikali nchini Kenya
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe, Mama Salma Kikwete, wakiwa katika hafla ya kutoa heshima zao na kuweka mashada ya maua kwenye kaburi la Mwanzilishi wa Taifa la Kenya, Hayati Jomo Kenyatta, jijini Nairobi Septemba 12, 2012, akiwa katika ziara rasmi ya Kiserikali (State Visit), ya siku tatu ambayo ni ziara yake ya kwanza rasmi nchini humo, ingawa amefanya ziara kadhaa za kikazi nchini Kenya.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe, Mama Salma Kikwete, wakiwa katika hafla ya kutoa heshima zao na kuweka mashada ya maua kwenye kaburi la Mwanzilishi wa Taifa la Kenya, Hayati Jomo Kenyatta, jijini Nairobi Septemba 12, 2012, akiwa katika ziara rasmi ya Kiserikali (State Visit) ya siku tatu ambayo ni ziara yake ya kwanza rasmi nchini humo ingawa amefanya ziara kadhaa za kikazi nchini Kenya.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe, Mama Salma Kikwete, wakiwa katika hafla ya kutoa heshima zao na kuweka mashada ya maua kwenye kaburi la Mwanzilishi wa Taifa la Kenya, Hayati Jomo Kenyatta, jijini Nairobi Septemba 12, 2012 akiwa katika ziara rasmi ya Kiserikali (State Visit) ya siku tatu ambayo ni ziara yake ya kwanza rasmi nchini humo ingawa amefanya ziara kadhaa za kikazi nchini Kenya.
Mama Salma Kikwete akiweka mashada ya maua kwenye kaburi la Mwanzilishi wa Taifa la Kenya, Hayati Jomo Kenyatta, jijini Nairobi Septemba 12, 2012 akiwa katika ziara rasmi ya Kiserikali (State Visit) ya siku tatu ya Rais Dk. Jakaya Kikwete, ambayo ni ziara yake ya kwanza rasmi nchini humo, ingawa amefanya ziara kadhaa za kikazi nchini Kenya.
Rais Kikwete akiangalia ng’ombe wanaofugwa kisasa katika shamba la kiwanda cha Brookside Diary.
Rais Kikwete akiangalia kondoo wanaofugwa kisasa katika shamba la kiwanda cha Brookside Diary.
Rais Kikwete akiangalia mchoro wa ujenzi wa jengo la kutengeneza maziwa ya unga la kiwanda hicho. Anayemuelekeza ni Mwenyekiti wa kampuni ya Brookside Diary, Muhoho Kenyatta.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka jiwe la msingi katika jengo jipya la kutengeneza maziwa ya unga katika Kiwanda cha Maziwa cha Brookside Diary, kwenye Barabara ya Thika, nje kidogo ya jiji la Nairobi. Kushoto ni Mwenyekiti wa kampuni ya Brookside Diary, Muhoho Kenyatta.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete akitembelea Chuo cha Taifa cha Ulinzi cha Kenya (National Defence College), kilichoko Karen, Nairobi, na baadaye kupiga picha ya pamoja na ujumbe wake, wanachuo na viongzozi wa chuo hicho.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete, akiwa katika picha ya pamoja na wenyeji wake baada ya kutembelea, Kituo cha Magonjwa ya Moyo na Kansa kwenye Hospitali ya Chuo Kikuu cha Aga Khan, jijini Nairobi Septemba 12, 2012, akiwa katika ziara rasmi ya Kiserikali (State Visit) ya siku tatu ambayo ni ziara yake ya kwanza rasmi nchini humo ingawa amefanya ziara kadhaa za kikazi nchini Kenya.
No comments:
Post a Comment