UVCCM wamaliza kikao cha Baraza
Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana (UVCCM), Martine Shigela akichangia ajenda katika kikao cha Baraza la Umoja huo. Katikati ni Makamu Mwenyekiti, Beno Malisa na Naibu Katibu Mkuu, Mfaume Kizigo, wakiwa katika kikao cha Baraza hilo, kililofanyika juzi, ukumbi wa sekretarieti maarufu kama (white house) uliopo Makao Makuu ya Chama, Dodoma.
Baadhi ya maafisa na Watendaji wa Umoja wa Vijana, wa kwanza kushoto ni Shara Ahmed (Mkuu wa Kitengo Cha Oganaizesheni Unguja), John Melele (Mkuu wa Kitengo cha Fedha na Uchumi), Deogratius Daffi (Mhasibu Mkuu) na Salmin Dauda (mwenye laptop), Mkuu wa Kitengo Cha Benki ya Vijana.
Mjumbe wa Kamati ya utekelezaji Taifa UVCCM, ambaye pia ni mjumbe wa kikao cha Baraza la Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ridhwan Kikwete, akichangia hoja katika kikao Cha Baraza hilo, kilichofanyika juzi, Makao Makuu ya Chama, mjini Dodoma.
Baadhi ya wajumbe wa Baraza la Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), wakiwa kwenye kikao cha baraza hilo.
Mjumbe wa Baraza la vijana (UVCCM), ambaye pia ni Mwenyekiti wa Vijana Mkoa wa Pwani na Mkuu wa Wilaya ya Kilwa, Abdalah Ulega, akichangia jambo katika kikao hicho, kilichofanyika juzi katika ukumbi wa Sekretarieti, Dodoma.
Wajumbe wa Baraza la Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi(CCM), wakifuatilia hoja kutoka kwa mmoja miongoni mwa wajumbe katika mjadala wa kupitisha majina ya wagombea wa nafasi mbalimbali ndani ya Umoja huo, ngazi ya Mkoa na Taifa.
No comments:
Post a Comment