Pichani juu ni Katibu Mkuu wa CPA, Dk. William Shijja, akihutubia wajumbe wa mkutano wa 58 wa CPA, mjini Colombo Sri Lanka. Pamoja na kutoa maelezo ya awali kuhusu shughuli zote za Mkutano huo wa Mwaka. Dk. Shija ni Katibu Mkuu Mtanzania wa CPA, ambaye anatumikia nafasi hiyo kwa kipindi cha pili sasa tangu 2007.
Spika wa Bunge, Anne Makinda akifuatilia moja wapo ya mada zilizokuwa zikiwasilishwa, wakati wa vikao vya mkutano wa 58 wa CPA, Mjini Colombo Sri Lanka leo. Pembeni yake ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama ya Bunge, Mussa Azzan Zungu. Waliokaa Nyuma ni Wabunge Zitto Kabwe na Muhonga Said Ruhwanya.
Ujumbe wa Tanzania katika Mkutano wa 58 wa CPA, ukifuatilia kwa makini baadhi ya mada zilikuwa zikiwasilishwa katika vikao vya Mkutano huo. Wa Kwanza kushoto ni Mbunge Zitto Kabwe, alieye kulia ni Muhonga Said Ruhwanya na nyuma ya Mbunge Zitto ni Hamad Rashid Muhamed ambao wote, kutoka Tanzania. (Picha zote na mdau wetu)
Thursday, September 13, 2012
Mkutano wa 58 wa Mabunge wanachama wa Jumuiya ya Madola (CPA), waendelea Colombo, Srilanka
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment