TANGAZO


Thursday, September 13, 2012

Serengeti yakabidhi vifaa vya kupimia kilevi kwa Jeshi la Polisi, kukabiliana na madereva walevi


Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchini (kulia), akipokea vifaa vya kupimia kilevi kwa madereva kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya bia ya Serengeti (SBL), Steve Gannon katika hafla ya makabidhia iliyofanyika Makao Makuu ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. Vifaa hivyo vina thamani ya shilingi milioni 60. Katika msaada huo, pia Kampuni ya bia ya Serengeti imetoa vitabu 20,000 vya leseni kwa ajili ya kusaidia wiki ya nenda kwa usalama barabarani, inayotarajiwa kuzinduliwa Kitaifa, siku ya jumatatu, mkoani Iringa. Kushoto ni Mkurugenzi wa Mawasiliano wa kampuni SBL, Teddy Mapunda. 
Mkurugenzi wa Mawasiliano Kampuni ya bia ya Serengeti, Teddy Mapunda, akizungumza katika hafla ya makabidhiano ya vifaa maalum vya kupimia ulevi kwa madereva. Wa pili kulia ni Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk. Emmanuel Nchimbi, kulia  Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Mbarak Abdulwakil na katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya bia ya Serengeti (SBL), Steve Gannon. 
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya bia ya Serengeti (SBL), Steve Gannon  akizungumza wakati wa makabidhiano hayo leo. Katikati ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi, kulia  Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Mbarak Abdulwakil.
Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohamed Mpinga, akijaribu moja ya kifaa hicho, jinsi ya kukitumia, huku Waziri  Emmanuel Nchimbi (katikati), Katibu Mkuu, Mbarak Abdulwakil (wa pili kulia), wakiangalia. Kushoto ni Mkurugenzi wa Mawasiliano Kampuni ya bia ya Serengeti, Teddy Mapunda na wa pili ni Mkurugenzi Mtendaji wa SBL, Steve Gannon. 
 Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya bia ya Serengeti (SBL), Steve Gannon, akionesha jinsi kifaa hicho kinavyofanya kazi, huku Waziri wa Mambo ya ndani, Dk. Emmanuel Nchimbi (katikati), Katibu Mkuu, Mbarak Abdulwakil (wapili kulia), Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohamed Mpinga (kulia), Meneja wa Miradi Endelevu na Uwajibikaji SBL, Nandi Mwiyombela (kushoto) na Mkurugenzi wa Mawasiliano Kampuni hiyo, Teddy Mapunda, wakiangalia.
Afande Agatha na Maafisa wenzake  mbalimbali wa Jeshi la Polisi, wakiwa katika hafla ya makabidhiano, yaliyofanyika Makao Makuu ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

No comments:

Post a Comment