TANGAZO


Wednesday, September 12, 2012

Waziri Magufulia akagua maendeleo ya Ujenzi wa Daraja la Kigamboni, marudio ya ujenzi Barabara ya Kilwa

Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli, akijiridhisha kwa kupima kiwango cha lami inayowekwa upya katika barabara ya Kilwa na Kampuni ya Kajima ya Japan leo, jijini Dar es Salaam. Wengine wanaoshuhudia kutoka kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Saidi Meck Sadiki, Balozi wa Japani nchini Tanzania, Masaki Okada na baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya Kajima. (Picha na Aron Msigwa -MAELEZO)

Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli (mbele), akiwa amefuatana na Balozi wa Japan nchini Tanzania, Masaki Okada, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam na viongozi wengine wa Wizara wakikagua moja ya sehemu ya barabara ya Kilwa, inayojengwa upya na Kampuni ya KAJIMA  ya Japan kutokana na barabara hiyo, iliyokamilika hapo awali kuwa chini ya kiwango na Serikali ya Tanzania kuikataa na kuiagiza Kampuni hiyo, iijenge upya kwa gharama zake.


Wafanyakazi wa Kampuni ya Kajima, wakiendelea na ujenzi wa barabara ya Kilwa leo, jijini Dar es salaam.


Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli (katikati), akimweleza jambo Balozi wa Japan nchini Tanzania, Masaki Okada (kushoto), wakati akikagua maendeleo ya ujenzi wa barabara ya Kilwa inayojengwa upya na Kampuni ya KAJIMA ya Japan leo, jijini Dar es Salaam. Kulia ni Naibu Waziri wa Ujenzi, Gerson Lwenge.


Mhandisi Mkazi wa Kampuni ya Kajima ya Japan, inayojenga upya barabara ya Kilwa, Hisashi Muto (kushoto), akitoa maelezo ya awali ya ujenzi wa barabara hiyo kwa Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli leo, jijini Dar es Salaam.


Wakazi wa eneo la Mbagala, wakimsikiliza Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli, wakati alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa barabara ya Kilwa leo, jijini Dar es Salaam. Pamoja na mambo mengine, amewataka wananchi kutoa ushirikiano kwa mkandarasi, kulinda miundombinu na kuacha tabia ya kujenga katika maeneo ya hifadhi ya barabara ili mradi huo ukamilike kwa wakati.


Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli akikagua ujenzi wa daraja la Kigamboni akiwa ameambatana na viongozi wa Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Saidi Mecki Sadiki (wa pili kulia), Mbunge wa Kigamboni, Dk. Faustine Ndugalile (wa tatu kulia) leo, jijini Dar es Salaam. Daraja la Kigamboni linajengwa na Kampuni ya China Railways Engineering kwa gharama ya shilingi bilioni 214 na linatarajia kukamilika kabla ya mwaka 2015.


Daraja la Kigamboni likiendelea kujengwa katika bahari ya Hindi, eneo la Kurasini. Daraja hilo, litakapokamilika litakua na njia 6 pamoja na barabara za juu na kuwa moja ya Daraja kubwa na la kipekee Afrika Mashariki na Kati.  


Mmoja wa wafanyakazi wa Kampuni inayojenga daraja hilo, ambaye jina lake halikupatikana mara moja, akiendelea na zoezi la kupiga picha huku akiwa amesimama kwenye mtambo unaopitisha umeme mwingi bila kuchukua tahadhari yoyote, wakati Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli, alipokuwa akikagua maendeleo ya ujenzi wa daraja hilo leo.

No comments:

Post a Comment