TANGAZO


Wednesday, September 12, 2012

Rais Jakaya Kikwete afanya ziara Kiserikali ya siku tau nchini Kenya


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete, akiwa na mwenyeji wake, Rais Mwai Kibaki wa Kenya pamoja na ujumbe wake, wakiingia Ikulu ya Nairobi  jana, 11 Septemba , 2012,  alipoanza ziara rasmi ya Kiserikali (State Visit) ya siku tatu nchini humo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete na mwenyeji wake, Rais Mwai Kibaki wa Kenya, wakipata picha ya kumbukumbu, Ikulu ya Nairobi  Jumanne, 11 Septemba, 2012, alipoanza ziara rasmi ya Kiserikali (State Visit) ya siku tatu nchini humo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete na mwenyeji wake, Rais Mwai Kibaki wa Kenya, wakipiga picha ya kumbukumbu, Ikulu ya Nairobi  Jumanne, 11 Septemba, 2012, alipoanza ziara rasmi ya Kiserikali (State Visit) ya siku tatu nchini humo. Kushoto ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Tanzania, Bernard Membe na kushoto ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya Profesa Sam Ongeri.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete na ujumbe wake pamoja na wenyeji, Rais Mwai Kibaki na ujumbe wake, wakiongea na wanahabari na kisha kupiga picha ya pamoja baada ya mazungumzo yao, rasmi ya Kiserikali kati ya nchi hizo mbili.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete na mwenyeji wake, Rais Mwai Kibaki wa Kenya, wakipongezana mara baada ya kuongea na waandishi wa habari, Ikulu mjini Nairobi jana.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete na mwenyeji wake, Rais Mwai Kibaki wa Kenya, wakipiga picha ya kumbukumbu, Ikulu ya Nairobi, jana Jumanne, Septemba 11, 2012, alipoanza ziara rasmi ya Kiserikali (State Visit) ya siku tatu nchini humo. Kushoto ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Tanzania, Bernard Membe na kushoto ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya Profesa Sam Ongeri.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete, akikata utepe kufungua rasmi jengo la Shule ya Ukarimu na Utalii ya Chuo Kikuu cha Kenyatta. Kulia kwake ni Waziri wa Elimu ya Juu, Margaret Kamar na kushoto kwake, ni Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Olive Mugendi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete, akitembezwa kuangalia shughuli mbalimbali zinazofanywa na wanafunzi baada ya  kufungua rasmi jengo la Shule ya Ukarimu na Utalii ya Chuo Kikuu cha Kenyatta.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete, akitembezwa kuangalia shughuli mbalimbali zinazofanywa na wanafunzi baada ya  kufungua rasmi jengo la Shule ya Ukarimu na Utalii ya Chuo Kikuu cha Kenyatta.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete, akitembelea na kujionea shughuli mbalimbali za Taasisi ya Utatifi wa Kilimo ya Kenya (KARI), jana. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete, wakiwa na  Rais Mwai Kibaki, Waziri Mkuu wa Kenya, Raila Odinga (kushoto) na Makamu wa Rais  wa Kenya, Kalonzo Musyoka kabla ya dhifa ya Kitaifa  waliyoandaliwa na mwenyeji wao.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na ujumbe wake na wenyeji wao, wakianza mazungumzo rasmi ya Kiserikali kati ya nchi hizo mbili.
Rais Mwai Kibaki wa Kenya, akiongea wakati wa dhifa ya Kitaifa aliyomwandalia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete Hoteli ya Inter Continental.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete, akijibu hotuba na baadaye kunyanyua glasi juu, kuwatakia afya njema wenyeji wake, wakati wa dhifa ya Kitaifa iliyoandaliwa kwa heshima yake, Hoteli ya Inter Continental.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete, akigonganisha glasi na Rais Mwai Kibaki wakati wa dhifa ya Kitaifa, Hoteli ya Inter Continental. (Picha zote na Ikulu)

No comments:

Post a Comment