Mama Mwanamwema Shein, afungua kituo cha Polisi Fumba, Zanzibar
Mke wa Rais wa Zanzibar, Mama Mwanamwema Shein, akikata utepe, ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa Kituo cha Polisi cha Fumba, Mkoa wa Mjini Magharibi, kisiwani Zanzibar leo. Kulia ni Mkuu wa Mkoa huo, Abdalla Mwinyi Khamis na Kamishna wa Polisi Zanzibar, Mussa Ali Mussa. (Picha zote na Ramadhan Othman Ikulu)
Mke wa Rais wa Zanzibar, Mama Mwanamwema Shein, akipata maelezo kutoka kwa Kamishna wa Polisi Zanzibar, Mussa Ali Mussa, alipokitembelea Kituo cha Polisi cha Fumba, Mkoa Mjini Magharibi leo, baada ya kufanya ufunguzi rasmi wa kituo hicho, kilichojengwa na jeshi hilo. Katikati ni mke wa Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mama Pili Seif Iddi.
Baadhi ya Maofisa mbalimbali wa Jeshi la Polisi Zanzibar, wakimsikiliza Mke wa Rais wa Zanzibar, Mama Mwanamwema Shein, akizungumza na wananchi wakati wa sherehe za ufunguzi wa Kituo cha Polisi cha Fumba, Mkoa wa Mjini Magharibi leo.
Baadhi ya Maofisa mbalimbali wa Jeshi la Polisi Zanzibar, wakimsikiliza Mke wa Rais wa Zanzibar, Mama Mwanamwema Shein, alipokuwa akizungumza na wananchi wakati wa sherehe za ufunguzi wa Kituo ha Polisi cha Fumba, Mkoa wa Mjini Magharibi leo.
Mke wa Rais wa Zanzibar, Mama Mwanamwema Shein, akimkabidhi cheti Mkurugenzi wa Biashara na Huduma kwa wateja, Mussa Ramadhan Haji kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maji (ZAWA), ikiwa ni miongoni mwa waliochagia katika ujenzi wa Kituo cha Polisi cha Fumba, kilichopo Mkoa Mjini Magharibi Unguja, wakati wa hafla ya ufunguzi wa kituo hicho leo.
No comments:
Post a Comment