TANGAZO


Sunday, September 16, 2012

Vurugu zazuka uchaguzi mdogo Jimbo la Bububu mjini Zanzibar




 Kumekuwa na vurugu za hapa na pale, Polisi kupambana na vijana kwenye kituo cha kupigia kura wakati wa  uchaguzi mdogo kumchagua Mwakilishi wa Jimbo la Bububu mjini Zanzibar leo.

 

Polisi wa kuzuia ghasia (FFU), wakisaidiwa na kikosi cha Valantia wakilinda kwenye mitaa ya Bububu huku wakiwaondoa vijana   waliojikusanya karibu na kituo cha kupigia kura  kwenye  Shule ya Bububu.




Kijana akiwa ameshikiliwa na Polisi wa FFU, kwenye Jimbo hilo.




Askari wa kikosi cha Kuzuiya Ghasia (FFU), wakivanjari na gari lao maeneo ya Bububu, mjini Unguja lao.

Askari wa kutuliza ghasia wakiwaondo vijana waliokuwa wamejikusanya vikundi kwenya eneo.
Vijana wakisalimu amri mbele ya Polisi, wakinyanyua mikono juu.
Askari wa Mafunzo, Valantia na JKU, wakishuka kwenye gari lao kwa ajili ya kulinda eneo la kupigia na kuhesabia kura.
 Baadhi ya mawakala wa vyama wakifuatilia upigaji kura.

 Kijana akitumbukiza kura yake kwenye kisanduku cha kupigia kura kwenye kituo cha Shule ya Bububu, mjini Zanzibar. 

Kiongozi wa chama cha siasa (kushoto), akizungumza na wandishi wa habari nje ya kituo cha kupigia kura.  (Picha zote na Martin Kabemba)
 

No comments:

Post a Comment