Warembo wanaowania taji la Redd’s Miss Temeke, litakalofanyika Ijumaa hii Sept 21, ukumbi wa PTA (Sabasaba Hall), wakiwasiliza wakufunzi wao. Kutoka kulia ni Joyce Maweda, Leyla Bhanji, Hawa Ismail na Mwajabu Juma, wakati wa mazoezi yao jana, Sigara Club, Chang'ombe jijini Dar es Salaam.
Wakufunzi wa warembo wanaowania taji la Redd’s Miss Temeke, litakalofanyika Ijumaa hii Sept 21, ukumbi wa PTA (Sabasaba Hall), wakiwafunda warembo hao jana, wakati wa mazoezi yao ukumbi wa Sigara Club, Chang'ombe jijini Dar es Salaam. Kutoka kulia ni Joyce Maweda, Leyla Bhanji, Hawa Ismail na Mwajabu Juma.
Warembo wanaowania taji la Redd’s Miss Temeke, wakiwa mazoezini leo kwenye Club ya Sigara (TCC), Chang’ombe Dar es Salaam. Shindano hilo litafanyika Ijumaa hii Sept 21, kwenye ukumbi wa PTA. (Picha zote na Intellectuals Communications Limited)
Na Mewandishi wetu
KAMATI ya Redds Miss Tanzania leo, inatarajiwa kutembelea kambi ya Redd’s Temeke 2012, kubwa ni kuwafunda vimwana hao kutoka Vitongoji vya Kigamboni, Kurasini na Chang’ombe, kuhusu mambo mbalimbali ndani ya mashindano ya urembo.
Kamati hiyo itaongozwa na Mkurugenzi wake, Hashim Lundenga atakayefuatana na mshauri wa masuala ya urembo katika kamati yao, Dk. Ramesh Shah, katibu Bosco Majaliwa, Mkuu wa Itifaki, Albert Makoye na mjumbe wa kamati hiyo, Lucas Rutta.
Shindano la Redd’s Miss Temeke, linafanyika Ijumaa hii katika ukumbi wa PTA(SabaSaba Hall) na tiketi za VIP zimeshaanza kuuzwa katika Club za City Sports Lounge iliyopo makutano ya Samora na Azikiwe na Nyumbani Lounge iliyopo maeneo ya Namanga ambapo VIP kwa mtu mmoja ni Tshs 50,000 na pia waweza nunua kwa meza moja ama ya watu 8 kwa laki 4 au watu kumi laki 5.
Warembo hao ni Agness Goodluck, Angela Gasper, Flaviana Maeda,Edna Sylvester, Catherine Masumbigana, Khadija Kombo, Neema Doreen, Flora Kazungu, Lilian Joseph, Elizabeth Peter, Elizabeth Boniphace, Jesca Haule, Zulfa Bundala, Mariam Ntakisivya na Esther Albert.
Mbali ya vinywaji vya Redd’s na Dodoma Wine, Miss Temeke pia imedhaminiwa na gazeti la Jambo Leo, katejoshy.blogspot.com, Mariedo Boutique, Push Mobile, City Sports Lounge, 100.5 Times FM, Kitwe General Traders, Global Publishers na 88.4 Cloud’s FM.
Shindano hili litakuwa ni miongoni mwa mashindano ya lala salama kabla ya kupata warembo watakaoungana na warembo wa kanda nyingine kuingia kambini kumtafuta mrembo wa Redds Miss Tanzania kwa Mwaka huu.
No comments:
Post a Comment