Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CME), kutoka Wizara ya Kazi na Ajira, Cosmas Msigwa, akisoma chapisho lenye maelezo ya Kanuni mbalimbali za Ajira na Mahusiano kazini leo Sept. 7,2012, jijini Dar es Salaam, mbele ya waandishi wa habari ( hawapo pichani), wakati wa semina ya siku moja kwa wanahabari kuhusu taratibu za kutatua migogoro ya kila siku na changamoto zake sehemu za kazi nchini, ambapo wanahabari kupitia vyombo vyao, waweze kusaidia kutoa elimu hii kwa waajiri na waajiriwa pamoja na jamii nzima ya Watanzania kwa ujumla kupitia vyombo vyao. (Picha zote na Mwanakombo Jumaa- MAELEZO).Mdau wa Habari kutoka (UPL), Noor Shija wa Gazeti la Uhuru, akichangia katika semina ya siku 1 kwa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Sept 7, 2012, kuhusu taratibu za kutatua migogoro ya kila siku na changamoto zake sehemu za kazi nchini.
Baadhi ya waandishi wa habari, wakipitia makabrasha katika semina ya siku moja jijini Dar es Salam, kuhusu taratibu za kutatua mogogoro ya kila siku na changamoto zake sehemu za kazi. Semina iliyoandaliwa na Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CME), Wizara ya Kazi na Ajira, ambapo CME, imeeleza kuwa tangu kuzinduliwa kwa TUME mwaka 2007 hadi - Juni 30, 2012, tume hiyo, imepokea migogoro 43,003 na kati ya hiyo migogoro 31,125, sawa na asilimia 72.3, imeshapatiwa ufumbuzi.
Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Usuluhishi na Maamuzi (CME), katikati mwenye suti, akiongea na waandishi wa habari jiji Dar es Salaam leo katika semina ya siku moja kwa wanahabari kuhusu taratibu za kutatua migogoro ya kila siku na changamoto zake sehemu za kazi nchini. Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CME) ni taasisi ya Serikali iliyoundwa chini ya sheria ya Taasisi za kazi na. 7 ya mwaka 2004.
No comments:
Post a Comment