TANGAZO


Friday, September 7, 2012

Miili ya Askari wa JWTZ waliokufa nchini Sudan yaagwa leo

Askari wa JWTZ, wakiwa wamebeba moja ya jeneza lenye mwili wa askari wa 3 wa jeshi hilo, waliofariki kwa ajali ya maji wakivuka mto Lamada, Sudani walikokwenda kulinda amani chini ya jeshi la Umoja wa Mataifa muda mfupi kabla ya kuiaga mili hiyo, Lugalo jijini Dar es Salaam leo.
 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ulinzi, akitoa heshima za mwisho kwa miili ya marehemu.
 
Mkuu wa Majeshi nchini, Devis Mwamunyange, akitoa heshima za mwisho kwa miili ya marehemu.
 
Mkuu wa Majeshi nchini, Devis Mwamunyange, akimfariji mke wa moja wa askari walifariki Bi. Fatuma Chunguile.
 
Askari wa JWTZ, wakiingiza miili ya marehemu katika gari tayari kwa safari ya kuelekea mikoani kwa ajili ya mazishi.
 
Mkuu wa Majeshi, Jenerari Davis Mwamunyange, akiongea na vyombo vya habari wakati wa kuaga miili ya wanajeshi waliopoteza maisha katika jeshi la kulinda amani nchini Sudan. (Picha zote na mdau wetu)
 
 

No comments:

Post a Comment