TANGAZO


Friday, September 7, 2012

Naibu Waziri Mkuu wa China atembelea sehemu za Kihistoria Zanzibar

Naibu Waziri Mkuu wa China, Hui Liangyu, akipunga mkono kuwaaga wenyeji wake baada ya kumaliza ziara yake ya Siku mbili mjini Zanzibar leo.
 
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi, akiagana na Mgeni wake, Naibu Waziri Mkuu wa China, Hui Liangyu, Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Amani Karume, mjini Zanzibar mara baada ya kumaliza ziara yake ya sku mbili leo.
 
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi (katikati), akipunga mkono kumuaga rasmi, Naibu Waziri Mkuu wa China, Hui Liangyu, aliyeondoka leo na kwenda Dare es Salaam baada ya kumaliza ziara yake ya siku mbili visiwani Zanzibar.
 
Naibu Waziri Mkuu wa China, Hui Liangyu akiangalia mizinga ya zamani, iliyokuwa ikitumika Zanzibar, wakati wa utawala wa Kisultani.
 
Naibu Waziri Mkuu wa China Hui Liangyu, akiangalia mambo ya kihistoria mbalimbali katika Nyumba ya Wananchi, Forodhani ikiwa ni miongoni mwa ziara yake ya Siku mbili visiwani Zanzibar.
 
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi, akibadilishana mawazo na Naibu Waziri Mkuu wa China, Hui Liangyu, baada ya kumaliza ziara yake ya siku mbili visiwani Zanzibar leo. (Picha zote na Yussuf Simai, Maelezo Zanzibar)

No comments:

Post a Comment