TANGAZO


Monday, September 10, 2012

Serengeti yachangia vifaa sh. 17.5 wiki ya Usalama Barabarani


Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohamed Mpinga, akipokea msaada wa fulana 1000 za kuhamasisha wiki ya usalama barabarani na vipeperushi 500 kutoka kwa Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL), Teddy Mpunda katika makabidhiano yaliyofanyika Makao Makuu ya Usalama Barabarani, jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Meneja Mipango Endelevu na Uwajibikaji wa Kampuni ya Serengeti, Nandi Mwiyombela.Vifaa hivyo vina thamani ya shilingi milioni 17.5 na Kampuni hiyo, imesema inaangalia uwezekano wa kuchapisha vipeperushi vingine kwa ajili ya Mkoa wa Dar es Salaam ambapo vya awali vitapelekwa mikoani.
Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohamed Mpinga akipokea msaada wa vipeperushi 500 kwa ajili ya kuhamasisha wiki ya usalama barabarani kutoka kwa Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL), Teddy Mpunda katika makabidhiano yaliyofanyika Makao Makuu ya Usalama Barabarani, jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Meneja Mipango Endelevu na Uwajibikaji wa Kampuni ya Serengeti, Nandi Mwiyombela.
Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani Kamanda Mohamed Mpinga, akizungumza katika makabidhiano hayo, wakati alipokuwa akitoa shukurani zake kwa Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL), jijini Dar es Salaam leo. Wanaofuatia ni Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL), Teddy Mpunda na Meneja Mipango Endelevu na Uwajibikaji wa Kampuni ya Serengeti, Nandi Mwiyombela.
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL), Teddy Mpunda  akizungumza katika makabidhiano hayo. Kushoto ni Meneja Mipango Endelevu na Uwajibikaji wa Kampuni ya Serengeti, Nandi Mwiyombela.

No comments:

Post a Comment