TANGAZO


Sunday, September 16, 2012

Mwenge wa Uhuru waingia Mkoa wa Iringa na kuanza mbio zake za kuhamasisha maendeleo

 Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Kanali Mstaafu Issa Machibya akiwasalimu wananchi wa Mkoa wa Rukwa waliojitokeza katika uwanja wa ndege wa Sumbawanga kwa ajili ya kuupokea mwenge wa Uhuru ambao umemaliza mbio zake mkoani Kigoma na kuwasili mkoani Rukwa kwa ajili ya kuendelea na mbio zake katika Wilaya tatu za Sumbawanga, ambazo ni Kalambo na Nkasi kwa muda wa siku nne.

Kiongozi wa mwenge Kitaifa mwaka 2012, Kapteni Honest Ernest Mwanossa akiwa na wenzake pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Kigoma wakifanya maandalizi ya kuukabidhi Mwenge wa Uhuru kwa uongozi wa Mkoa wa Rukwa.
Baadhi ya viongozi wa Mkoa wa Rukwa kutoka kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Methew Sedoyyeka, Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Samson Mashalla, Mkuu wa Wilaya ya Nkasi na RPC wakishuhudia mapokezi hayo.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Injinia Stella Manyanya akipokea Mwenge wa Uhuru kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Kanali Mstaafu Issa Machibya mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa mjini Sumbawanga leo.
Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga, Mathew Sedoyyeka akipokea Mwenge wa Uhuru kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Injinia Stella Manyanya tayari kwa kuanza mbio zake katika wilaya hiyo ambapo baadaye utaenda Wilaya ya Kalambo na kumalizia katika Wilaya ya Nkasi.
Viongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa, wakiwa na viongozi wa Wilaya ya Sumbawanga wakikimbiza mwenge katika moja ya barabara za Manispaa hiyo, ikiwa ni kuunga Mkono na kukagua mradi wa Sumbawanga Ng’ara ambao lengo lake kuu ni kudumisha usafi katika Mji wa Sumbawanga. Mradi huo umeasisiwa na Mkuu wa Mkoa huo Injinia Stella Manyanya na kuzinduliwa rasmi na Makamu wa Rais Mohammed Gharib Billal alipokuwa ziarani mkoani Rukwa.
Kiongozi wa mwenge Kitaifa mwaka 2012, Kapteni Honest Ernest Mwanossa akipandikiza Samaki katika bwawa la kufugia Samaki lililopo Mishamo katika Manispaa ya Sumbawanga alipofika kukagua ufugaji wa samaki. Nyuma yake ni waandishi wa habari wakiwa katika harakati za kutafuta taswira mwanana kwa ajili ya kufikisha ujumbe kwa wananchi.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Injinia Stella Manyanya akiwapa utaratibu wa waendesha Pikipiki (Bodaboda), namna ya kuupokea Mwenge wa Uhuru. Jumla ya waendesha Pikipiki 100, walishirikishwa katika mapokezi ya Mwenge huo wa Uhuru.

No comments:

Post a Comment