TANGAZO


Sunday, September 16, 2012

Mbunge Mwindau amwaga mabati kwa kwa wajasiriamali Tanga

 
 Mbunge wa Viti maalum, Amina Mwidau (CUF), akimkabidhi kadi aliyekuwa kada wa CCM Wilaya ya Muheza, Hamis Mgosi, leo Mjini Muheza. Wengine ni wajumbe wa kamati ya Utendaji ya CUF, Wilaya ya Muheza, ambao walishuhudia tukio hilo.
 Mbunge wa Viti maalum, Amina Mwidau (CUF), akimkabidhi mabati kumi yenye thamani ya Sh 170,000 ambayo, alikabidhi kwa kikundi cha wajasiriamali wa Gongagonga, kwa Diwani wa Mwanzange, Rashid Jumbe (CUF) leo. Wengine wanashudia ni wajasiriamali wa kikundi hicho.
 Mbunge wa Viti maalum, Amina Mwidau (CUF), akimkabidhi mpira wa pete kiongozi wa timu ya Netball ya Mwanzange Girls, Mkunde Ramadhani. Wengine wanaoshudia ni Diwani wa Ngamiani Kati, Habib Mpa (CUF), mwenye kofia na shati la mistari , pamoja na wanakikundi cha Gongagonga. 

 Mbunge wa Viti maalum, Amina Mwidau (CUF), akionyeshwa kazi zinazofanywa na kikundi cha wajasiriamali cha Gongagonga na Diwani wa Mwanzange, Rashid Jumbe (CUF) leo, jiji Tanga.

Na Mwandishi Wetu, Tanga
MBUNGE wa Viti Maalum Mkoa wa Tanga Amina Mwidau (CUF), amekabidhi mabati kwa kikundi cha gongagonga cha Mwanzange pamoja na vifaa vya michezo kama njia ya kuwawezesha wajasiriamali hao.
Akizungumza leo jiji hapa baada ya kukabidhi mabati hayo kwa diwani wa kata ya Mwanzange Rashid Jumbe (CUF), mbunge huyo alisema kuwa taifa haliwezi kuendelea bila kuandaa utaratibu mzuri wa kuwathamini wajasiriamali wadogo wadogo wa nchini.
Alisema mabati hayo kwa kikundio hicho ni sehemu ya ahadi yake kwa wajasiriliamali hao ambao walitaka wapatiwe bati kumi ili waweze kujenga banda ambalo litawasaidia kuwakinga na jua pamoja na mvua.
“Ninajisikia furaha kutoka ndani ya nafsi nyangu leo hii kuweza kuwakabidhi mabati haya yenye thamani ya Sh 170,000 kwa na ninajua huu ni mwanzo najua tutakutana tena ili kuweza kutekeleza na mengine zaidi.
“Kama mnavyofahamu kuwa taifa lolote ili liweze kuendelea ni lazima liandae mazingira mazuri kwa wajasiliamali wake hasa vijana nja wanawake ambao ndiyo nguvu kazi ya Taifa na kama nilivyokuja na kuaniambia niwaletee nini sasa nimeanza na utekelezaji wa ahadi yangu hii kwenu.
“Mbali an hatua hii sasa ninachowaomba anzeni harakati za kusajili Saccos, ili kuweze kukopesheka na taasisi za fedha name kama Mbunge wenu nitawasaidia kwa kulisimamia hili kwa nguvu zangu zote,” alisema Mwidau.
Kwa upande wake Diwani wa kata ya Mwanzage Rashid Jumbe (CUF), alimshuruku mbunge huyo kutekeleza ahadi yake kwa wakati huku akiamuahidi atahakikisha nasimamia utekelezaji wa uanzishwaji wa Saccos kwa wajasiriamali wa Gongagonga.
“Ninajua wapo wengi lakini mbunge wetu Mwidau, umeonyesha mfano wa kuigwa kwani umeweza kutekeleza hili katika kipindi kifupi tangu ulipokuja hapa na kuzungumza na wajasiriamali hawa,” alisema Jumbe.

No comments:

Post a Comment