Mkutano wa Kamati Kuu ya CCM Dodoma
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete (katika), Rais wa Serikali ya Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Dk. Ali Mohamed Shein, Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Willson Mukama, Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Pius Msekwa kwa pamoja wakiimba wimbo wa chama hicho, walipoingia katika ukumbi wa Mkutano kabla ya kuanza kwa kikao cha Kamati Kuu leo, mjini Dodoma. (Picha zote na Ramadhan Othman, Dodoma)
Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Tanzania, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete (katika), Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Dk. Ali Mohamed Shein (kushoto), Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Willson Mukama (kulia), wakifurahia jambo wakati Mwenyekiti Kikwete, alipokuwa akiendesha kikao cha siku moja cha Kamati Kuu, kilichofanyika leo, ukumbi wa White House, Dodoma.
Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Tanzania, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete (kulia) na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Dk. Ali Mohamed Shein, wakifurahia jambo katika Kikao cha siku moja cha Kamati Kuu, kilichofanyika leo katika ukumbi wa White House, mjini Dodoma.
Wajumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa, wakiwa katika ukumbi wa Mkutano kabla ya kuanza kwa kikao hicho leo, kilichoendeshwa na Mwenyekiti wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Jakaya Mrisho Kiwete.
No comments:
Post a Comment