TANGAZO


Wednesday, September 12, 2012

Mkutano wa 58 wa Mabunge wanachama wa Jumuiya ya Madola (CPA), wafunguliwa Colombo, Srilanka


Spika wa Bunge, Anne Makinda akiwasili katika ukumbi wa Mnelum Pokuna Mahinda Rajapaksa, kuhudhuria ufunguzi rasmi wa Mkutano wa 58 wa chama cha Mabunge wanachama wa Jumuiya ya Madola (CPA), uliofunguliwa leo na Rais wa Sri Lanka, Mahinda Rajapaksa.  Aliye pembeni yake ni mjumbe wa CPA, tawi la Tanzania na Mbunge wa Kigoma, Zitto Kabwe.
  Rais wa Sri Lanka, Mahinda Rajapaksa, akihutubia Maspika, Wabunge na Maofisa zaidi ya 850, kutoka Mabunge ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Madoloa, wakati wa ufunguzi wa mkutano huo.
Spika wa Bunge, Anne Makinda akishangaa jambo wakati wakiwa katika mazungumzo na Spika wa Kenya, Kenneth Marende mara baada ya ufunguzi wa Mkutano wa 58 wa Bunge la CPA, unaofanyika nchini Sri Lanka.
Mbunge Zitto Kabwe, akiteta jambo na Mbunge wa Uganda (hakufahamika jina mara moja) pamoja na Spika wa Bunge la Malawi, Henry Chimundu Banda (katikati), mara baada ya ufunguzi wa Mkutano wa 58 wa Bunge la CPA, unaofanyika nchini Sri Lanka. Kulia ni Mbunge wa Wawi Pemba, Hamad Rashid ambaye ni Mjumbe wa CPA tawi la Tanzania.
Wajumbe wote wa Mkutano, wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya ufunguzi huo leo.
Spika wa Bunge, Anne Makinda (katikati), akiteta jambo na Spika wa Baraza la Wawakilishi, Pandu Ameir Kificho pamoja na Mbunge Zitto Kabwe, wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa 58 wa Chama cha Mabunge wanachama wa Jumuiya ya Madola (CPA), leo Mjini Colombo, Sri Lanka. Mkutano huo umefunguliwa rasmi na Rais wa Sri Lanka Mahinda Rajapaksa. Kulia kwa Spika Makinda ni Mbunge Mussa Zungu wa CPA tawi la Tanzania.
Spika wa Bunge, Anne Makinda (katikati), akiteta jambo na Spika wa Baraza la Wawakilishi, Pandu Ameir Kificho pamoja na Mbunge Zitto Kabwe, wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa 58 wa Chama cha Mabunge wanachama wa Jumuiya ya Madola (CPA), leo Mjini Colombo, Sri Lanka. Mkutano huo umefunguliwa rasmi na Rais wa Sri Lanka Mahinda Rajapaksa. Wa Kwanza kulia ni Afisa dawati wa CPA, tawi la Tanzania, Said Yakubu.

No comments:

Post a Comment