Waandishi wa habari wakiwa wamelibeba jeneza lenye mwili wa aliyekuwa mwandishi wa habari wa Televisheni ya Chanel Ten, mkoani Iringa, Daud Mwangosi, wakielekea makaburini, wakati wa mazishi yake yaliyofanyika nyumbani kwao Itete, wilayani Rungwe, mkoani Mbeya leo. Wachungaji wakifanya ibada ya mwisho kabla ya kuanza maziko ya marehemu Mwangosi.
Waombolezaji wakilishusha jeneza lenye mwili wa marehemu Daudi Mwangosi wakati wa mazishi yake.
Jenenza lenye mwili wa Marehemu Daudi Mwangosi likiwa limeshushuwa ndani ya Kaburi.
Waombolezaji wakifukia kaburi la marehemu Mwangosi mara baada ya jenenza lake kushushwa ndani ya kaburi.
Waombolezaji wakimalizia shughuli za kufukia kuburi la marehemu Mwangosi wakati wa mazishi, nyumbani kwao Mbeya leo.
Mke wa Marehemu Daudi Mwangosi, akiweka shada la mauwa kwa machungu.
Mke wa marehemu Mwangosi, akiwa amelala kwenye kaburi alilozikwa mumewe, huku akilia kwa uchungu.
Watoto wa marehemu Mwangosi, wakiweka mashada ya maua kwenye kaburi la baba yao.
Ni vigumu sana kuamini kwa mke wa marehemu, lakini hali ndivyo ilivyo kuwa akiwa na huzuni kubwa.
Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willibroad Slaa, akiweka shada la mau kwenye kaburi la marehemu Mwangosi.
Dk. Slaa, akiwa na viongozi wengine wa chadema, mara baada ya kuweka shada la maua.
Waziri Nchi, Ofisi ya Rais asiye na Wizara maalum, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Rungwe Mashariki, Profesa Mark Mwandosya na mkewe Lucy, wakiweka shada la maua juu ya kaburi la Mwangosi.
Rais wa UTPC akiweka shada la maua.
Ndugu wa marehemu Mwangosi, akiweka shada la maua kwenye kaburi lake.
Mwenyekiti wa Mbeya Press Club, naye akiweka shada la maua.
Ndugu wa marehemu Mwangosi, akiweka shada la maua kwenye kaburi lake.
Mwenyekiti wa Mbeya Press Club, naye akiweka shada la maua.
Mwandishi Mkuu wa Mbeya yetu, Joseph Mwaisango, akiwa anatoa heshima zake za mwisho katiaka kaburi la marehemu Mwangosi.
Waombolezaji na wananchi mbalimbali, wakirejea majumbani kwao baada ya kumalizika kwa shughuli za mazishi leo.
Waandishi wa habari wakichukua matukio moja kwa moja makaburini wakati wa mazishi ya marehemu Daudi Mwangosi leo.
`
`
Hapa waombolezaji wakiwa njiani kutoka makaburini kumzika mwanahabari wa Chanel Ten, Daudi Mwangosi leo. (Picha zote kwa hisani ya Mbeya yetu Blog)




















No comments:
Post a Comment