TANGAZO


Tuesday, September 11, 2012

Maandamano ya Waandishi wa Habari kulaani mauji ya mwenzao, Daudi Mwangosi


Katibu wa Jukwaa la wahariri, Nevil Meena akizungumza kabla ya kuanza kwa maandamano ya kulaani mauaji ya mwandishi wa habari wa kituo cha Channel Ten, marehemu Daudi Mwangosi. Maandamano hayo yalianzia katika Ofisi za Channel Ten na kuishia katika viwanja vya Jangwani.
 
Maandamano yakianza
 
Waandamaji wakielekea katika viwanja vya Jangwani jijini Dar es Salaam kulaani mauaji ya mwandishoi wa Channel Ten, marehemu Daud Mwangozi.
 
Waandamanaji wakiwa na mabango yao .
 
Wanahabari wa Tanzania, wakiwa barabara ya Morogoro wakielekea Jagwani yalikoishia maandamano yao.
Wanahabari wa Tanzania, wakionesha picha ya Mwangosi aliyeuawa na baadhi ya mabango ya kulaani mauaji hayo wakiwa barabara ya Morogoro wakielekea Jagwani yalikoishia maandamano yao.
Wanahabari wa Tanzania, wakionesha mabango ya kulaani mauaji hayo wakiwa barabara ya Morogoro wakielekea Jagwani yalikoishia maandamano yao.
Wanahabari wakionesha mabango yenye ujumbe mbalimbali kwenye maandamano hayo.
 
Katibu wa Jukwaa la Wahariri, Nevil Meena akizungumza katika viwanja vya Jangwani.
 

No comments:

Post a Comment